The House of Favourite Newspapers

ZARI, PETER WA P SQUARE MAMBO NI MOTO

DAR ES SALAAM: Mambo ni moto! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mjasiriamali Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kudaiwa kuwa ‘klozi’ na staa wa muziki kutoka Nigeria ambaye pia ni pacha wa Kundi la P Square, Peter Okoye ‘Mr. P’, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.

 

TUJIUNGE UGANDA

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Zari amekuwa na mawasiliano ya karibu na Mr. P licha ya kuwa staa huyo ana mke na watoto. “Zari amekuwa mtu wa kufanya siri sana tangu aachane na Diamond, miongoni mwa wasanii wanaomfariji kwa sasa ni Mr. P lakini hawataki mambo yao yajulikane,” kilisema chanzo.

AMEMJIBU DIAMOND?

Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, licha ya Diamond kuendelea kufanya mambo ambayo pengine anadhani anamkomoa kumbe anajikomoa mwenyewe.

“Juzijuzi kwenye mitandao kulichafuka baada ya Diamond kumsema vibaya Zari kuwa sijui ni kima na maneno mengine mengi ya dharau halafu mara tukaona sijui yeye na familia yake wamembeba mtoto wa Mobeto, sasa Zari yeye alishanawa mikono tangu zamani anamchora tu, yeye yupo bize na mambo yake.”

ATUA ZIMBAMBWE

Kama hiyo haitoshi, chanzo kinazidi kunyetisha kuwa, hivi karibuni Zari alitua Harare nchini Zimbabwe kwa ajili ya kusaini dili nono lakini siku moja kabla hajasaini dili hilo aliingia klabu ya usiku na wenzake na muda mwingi alikuwa akichati na Mr. P  “Akiwa klabu alinaswa akichati na Mr. P na kuna wakati DJ alipiga wimbo wa Mr. P wa Wokie Wokie, Zari akainuka na kuanza kucheza kwa hisia kali,” kilisema chanzo hicho.

AZUA MIJADALA

Mara baada ya klip na picha zikimuonesha Zari akiwa katika picha ya pamoja na Mr.P, mijadala ilianza kuzuka na wengine wakienda mbali zaidi kwa kusema wawili hao ni wapenzi. Baadhi ya mitandao nchini Uganda ilichafuka kwa kuwahusisha kuwa wawili hao wana uhusiano licha ya wenyewe kutozungumza lolote

TURUDI KWA ZARI

Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Zari aliweka Video ya Wokie Wokie na kusindikiza na maneno ya kumpongeza Mr. P na kueleza kwamba anaupenda sana wimbo huo: “My song of the moment @ peterpsquare killed it OMG WOKIE WOKIE full video link in his Bio @ peterpsquare u never disappoint bruh.”

 

Baada ya kuweka video na ujumbe huo, mwanamuziki Peter alikomenti kwa Zari na kumshukuru kwa kuikubali kazi yake ambapo aliandika kwa Kingereza ‘thanks my dear, I really appreciate.’  Kitendo hicho kilichochea zaidi mjadala kwa watu kuhoji kwamba urafiki huo ni zaidi ya ule wa kawaida kwani hata Diamond ameachia wimbo mpya (Jibebe) lakini mrembo huyo hajauposti.

 

TULIPOTOKA

Diamond alikuwa katika uhusiano na Zari uliozaa watoto wawili, Nillan na Tiffah. Waliachana Februari, mwaka huu na tangu hapo, Diamond amekuwa akihaha kurudisha penzi lao bila mafanikio.

STORI: Andrew Carlos,Risasi Mchanganyiko

Comments are closed.