Zelensky Amuangukia Rais wa China Kutatua Vita Yake na Putin
RAIS wa Ukraine Volodimir Zelensky ameomba kwa mara nyingine kuonana ana kwa ana na Rais wa Jamhuri ya China Xi Jinping ili kufanya mazungumzo ambayo yatasaidia kutatua vita kati ya nchi yake ya Ukraine na Urusi.
Zelensky amebainisha kuwa amekuwa akiomba kuongea na Jinping tangu vita bhiyo ilipoanza mwezi Februari mwaka huu ingawa imekuwa ngumu kwa jambo hilo kutimia.
Zelensky amesema kuwa anatamani kuona China inatumia uhusiano wake wa kidplomasia pamoja na nguvu ya kiuchumi kuishawishi Urusi kusitisha mapigano ndani ya nchi hiyo.
“Ningependa kuongea naye ana kwa ana, nilipata fursa ya kuongea na Rais Xi Jinping mara moja lakini hiyo ilikuwa ni mwaka mmoja uliopita. Tangu kuanza kwa uvamizi mkubwa Februari 24, tumeomba mazungumzo rasmi lakini hatujafanikiwa kupata nafasi hata mara moja ya kuongea na China licha ya kwamba naamini kungekuwa na msaada.” alinukuliwa Zelensky akikiambia chombo cha habari cha Zoom kilichopo Hong Kong.
China ni mshirika mkubwa wa Urusi ambaye hadi sasa hajakemea uvamizi wa Urusi katika nchi ya Ukraine akisisitia kuwa oparesheni ya Urusi nchini Ukraine imesababishwa na uchochezi wan chi za Magharibi hasa mataifa yanayounda Jumuiya ya NATO.
Hadi sasa tangu vita hiyo ianze jumla ya watu 5,327 wameripotiwa kuuawa na zaidi yaw engine milioni 12 wakilazimika kukimbia makazi yao.