Zelinsky Kusafiri Hadi Sauz Kukutana Na Ramaphosa
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky anatarajiwa kusafiri hadi Pretoria, Afrika Kusini kwenda kukutana na Rais Cyril Ramaphosa mnamo April 10, 2025.
Msemaji wa Rais Ramaphosa, Vincent Magwenya ameliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa Zelensky anatarajiwa kwenda kujadiliana na Ramaphosa kuhusu mpango wa Marekani kusitisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine sambamba na kutafuta suluhu ya kudumu kati ya nchi hiyo na Urusi.
Ikumbukwe kuwa Afrika Kusini ilichagua kutoegemea upande wowote tangu kuanza kwa Vita vya Ukraine ambapo Rais Ramaphosa amewahi kukutana na Rais Vladmir Putin na baadaye Zelensky katika jitihada za kujaribu kuwapatanisha.