The House of Favourite Newspapers

Zenji yaichapa Kenya, Kili Stars uwanjani leo

zanzibar heroesNa Mwandishi Wetu, Awassa

ZANZIBAR haijakubali kutolewa kinyonge kwenye michuano ya Kombe la Chalenji kwani jana Ijumaa iliifunga Kenya mabao 3-1, kwenye Uwanja wa Awassa, Ethiopia.

Katika mchezo huo uliokuwa wa mwisho kwa Kundi A, mabao ya Zanzibar Heroes yalifungwa na Suleiman Kassim ‘Selembe’ aliyefunga mawili dakika ya 44 na 73 na lingine likifungwa na Hamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 56. Bao la kufutia machozi la Kenya lilifungwa na Jacob Kell dakika ya 91.

Pamoja na ushindi huo, Heroes imetupwa nje baada ya kufungwa katika mechi zake mbili za awali dhidi ya Burundi na Uganda.

Katika hatua nyingine, kikosi cha Kilimanjaro Stars, leo Jumamosi kitashuka uwanjani kupambana na wenyeji wa michuano hiyo, Ethiopia.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa lakini matokeo yoyote hayatakuwa na madhara kwa Kilimanjaro Stars kwani tayari imeshatinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kushinda mechi zake mbili za awali dhidi ya Somalia na Rwanda.

Comments are closed.