testiingg
The House of Favourite Newspapers

ZIC Watoa Zawadi ya Bodaboda Kwa wakala Bora

0

Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) limetoa zawadi ya Piki piki kwa wakala wake Sunshine Insurance Agency kama njia ya kuthamini mchango wake na jitihada aliyoonesha katika mwezi wa Aprili, 2023.

Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) linatarajia kuadhimisha miaka 54 Tangu kuanzishwa kwake ifikapo Juni 20, mwaka huu. Katika kuhakikisha wanaendelea kuwanyanyua mawakala wao Shirika limekuja na mpango wa kutoa pikipiki kwa kila wakala ambae atafanya vizuri zaidi katika kila mwezi.

Katika hafla ya kukabidhi pikipiki hiyo kwa Sunshine Insurance Agency, Meneja wa (ZIC) Kanda ya Ziwa Bahatisha Suleiman amewapongeza washindi hao kwani jitihada zao binafsi ndiyo zilizopelekea kushinda zawadi hiyo.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Shirika la Bima la Zanzibar Mohamed Shaaban amesema zawadi hii itakwenda kuwa chachu ya jitihada kwa mawakala wengine ambao nao wana nafasi ya kujishindia pikipiki katika miezi ijayo.

Hata hivyo Uongozi wa Sunshine Insurance Agency kupitia Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Happiness Lyatuu Mkelemi wametoa shukurani zao za dhati kwa kupatiwa zawadi hiyo na wameahidi kuendelea kuwahudumia wateja wa Shirika la Bima la Zanzibar kama dira na mikakati ya Shirika hilo inavyoelekeza.

Leave A Reply