Zidane Ampigia Salute Guardiola

KOCHA Mkuu wa klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amemwangia sifa kocha wa Manchester City, Pep Guardiola na kusema ni miongoni mwa makocha bora. Zidane amesema Guardiola ni kocha bora anaemuheshimu kutokana na ubora aliokuwa nao.

 

“Pep amekuwa bora kwenye timu nyingi ambazo amefundisha alikuwa Barcelona kisha Bayern Munich na sasa yupo Manchester City kwa maoni yangu, yeye ni kocha bora. Watu wengine watafikiria kumtaja kocha mwingine lakini kwangu mimi kocha bora ni Pep Guardiola kwa sababu ya ubora aliyokuwa nao” alisema Zidane.

 

Real Madrid na Manchester City zitakuwa uwanjani leo kwenye mchezo wa raundi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaopigwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.


Loading...

Toa comment