The House of Favourite Newspapers

Zidane Kurudisha Samba Real Madrid

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amepania kuona timu yake ikicheza soka la kuvutia la pasi aina ya samba ambalo huchezwa zaidi nchini Brazil.

 

Zidane anaamini katika siku za karibuni Real Madrid imekuwa haivutii katika uchezaji wake. Dalili za hali hiyo ni kitendo chake cha kumsajili dogo wa kibrazili, Rodrygo kwenye kikosi chake.

 

Rodrygo ameweka rekodi ya kuwa staa wa 26 wa kibrazili kuwahi kuchezea Real Madrid ambayo ilianzishwa miaka 117 iliyopita.

 

Brazil ni nchi ya pili kwa kutoa wachezaji wengi kwa timu hiyo, ambapo Argentina inaongoza kwani mastaa wake 28 wamewahi kukipiga katika timu hiyo.

 

Zidane sasa amepania kuona timu yake ikicheza soka safi la pasi ambalo huko Brazil huitwa samba ili kuweza kuvutia duniani kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Ndio maana kikosi chake sasa kina wabrazili watano Militao, Marcelo, Casemiro, Vinicius na Rodrygo. Zidane amerudisha historia ya msimu wa 2005/06 wakati Real Madrid ilipokuwa na wabrazili Roberto Carlos, Ronaldo, Baptista, Robinho na Cicinho.

 

Wabrazili hao sasa wanatazamiwa kuchanganyika na mastaa wengine wapya katika kikosi hicho kama Eden Hazard, Ferland Mendy na Luka Jovic na kuifanya Real Madrid kuwa moto msimu ujao.

Comments are closed.