The House of Favourite Newspapers

Zigo la Euro Na Hisense Yafikia Tamati Wananchi Wakinufaika na Zawadi Lukuki

0

Dar es Salaam, 19 Julai 2024: Kampeni ya Zigo la Euro na Hisense iliyokuwa ikiendeshwa na Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo na kuwanufaisha wananchi mbalimbali kwa zawadi za pesa taslimu, vifaa vya kielekroniki ambavyo ni friji na runinga za kisasa kutoka kampuni ya Hisense leo imehitimishwa rasmi.

Akizungumza kwenye hafla ya kuhitimisha kampeni hiyo, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Ruta amesema katika kampeni washindi walikuwa wakijishindia zawadi hizo kwa kufanya miamala kwa kutumia Tigo Pesa Super App au kubeti kwa kutumia Kampuni ya Pari Match ambapo washindi 47 walinufaika na zawadi mbalimbali.

Meneja huyo alisema katika washindi hao kuna washindi 7 walikwenda kujionea fainali za Euro 2024 nchini Ujerumani, washindi 16 walijishindia shilingi milioni moja moja, washindi 24 walijishindia vifaa vya kielekroniki kutoka kampuni ya Hisense ambavyo ni friji na runinga ya kisasa.

Katika tukio hilo washindi watatu wa na wa mwisho walikabidhiwa zawadi zao.

Akihitimisha kampeni hiyo Mary alisema;

“Kampeni hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa sana wateja wetu kutumia App yetu hii mpya na ya kijanja ya Tigo Pesa Super App ili wajipatie huduma bora.

“Nitumie nafasi hii kuwapongeza washindi wote walijishindia zawadi hizo na kuwataka waliojaribu na kushindwa wasikate tamaa kwani Tigo kama kawaida yake mwisho wa kampeni hii ndiyo mwanzo wa jambo jingine”. Alimaliza kusema.

Leave A Reply