The House of Favourite Newspapers

Zijue njia 10 za kuwa tajiri kama Dangote

0

Business magnate man Aliko Dangote, ranked by Forbes Magazine as the richest man in Africa, speaks during a send off ceremony of 250 Nigerian health workers on a mission to fight Ebola virus in affected West African countries and launch of African initiative operating under the hash tag #AfricaAgainstEbola in Lagos on December 3, 2014. Two hundred and fifty volunteer Nigerian medical corps under the auspices of the African Union Support to Ebola Outbreak in West Africa (ASEOWA) were given a send off to fight Ebola Virus Diseases in the affected three West African countries of Liberia, Sierra Leone and Guinea. The African Union, which is collaborating with the private sector to raise funds to support and strengthen the Unions response to the crises, is sending more than 1000 health workers before Christmas. AFP PHOTO/PIUS UTOMI EKPEI (Photo credit should read PIUS UTOMI EKPEI/AFP/Getty Images)

Alhaji Aliko Dangote.

BARANI Afrika kuna mtu anayetajwa kuwa tajiri namba moja akiwa na kitita cha Dola za Kimarekani bilioni 15.4 (zaidi ya Sh. trilioni 33 za Kibongo).

Huyu si mwingine ni Alhaji Aliko Dangote, raia wa Nigeria. Biashara zake zimesambaa katika nchi nyingi Afrika ikiwemo Tanzania, akisambaza bidhaa nyingi kama sementi na sukari. Dangote alianza biashara yapata miaka 30 iliyopita na bado anaendelea kujitanua kila kukicha.

Wakati anaanza, mtu huyu alikopa fedha kidogo za mtaji kutoka kwa mjomba’ke aliyekuwa amemwajiri. Akamkopesha kwa makubaliano kuwa azirudishe baada ya miezi mitatu. Ili kujijengea uaminifu, Dangote alirejesha mkopo huo kabla ya miezi hiyo mitatu kumalizika.

Alianza na biashara mbalimbali. Kilichomsaidia ni kubuni mfumo wa usambazaji bidhaa uliokuwa wa haraka kushinda washindani wake. Tumchukue Dangote kama mfano, tuone njia kumi  10) zilizomsaidia hadi akafi kia kwenye kilele cha mafanikio, naamini njia hizi zinaweza kukufungua na wewe ukapata utajiri kama yeye. Dangote mwenyewe huwa hapendi kufi cha, huzisema waziwazi kila anapokuwa na fursa ya kuzungumza na watu kuhusiana na mafanikio yake;

1: ZALISHA, USIWE MCHUUZI
Dangote alianza biashara zake kama mchuuzi wa bidhaa wa kawaida kabisa kama unavyoona hapa kwetu wafanyabiashara wadogowadogo wakinunua bidhaa kama nguo, viatu, mafuta na nyinginezo kisha kwenda kuchuuza kwa faida. Kadiri alivyokuwa akikua, alijipatia uzoefu mkubwa kibiashara na hali ya kujiamini. Kwenye simulizi yake ya mafanikio, mara nyingi hupenda kuweka bayana kwamba, mafanikio yake makubwa kibiashara yametokana na kuhama kutoka uchuuzi wa bidhaa na kuwa mzalishaji wa bidhaa.

Dangote mwenyewe anasema, ‘zalisha na siyo kufanya uchuuzi tu, kuna fedha nyingi kwenye uzalishaji, ingawa unahitajika uwekezaji mkubwa. Ili nitoke, nililazimika kuanza kuzalisha bidhaa kama zilezile nilizokuwa nikizichuuzi. Mimi natetea uzalishaji kwa sababu siyo tu uzalishaji unazidisha hadhi yako katika biashara, bali pia unakusaidia wewe kama mjasiriamali kurudisha kile ulichokipata kwa jamii yako na nchi kwa jumla kwa njia ya kuongeza nafasi za ajira na maendeleo ya kiuchumi’.

2: JENGA JINA NA KAMWE USILIHARIBU

Hii ni njia au mbinu ya pili ya mafanikio ya Dangote ambaye ni muumini mzuri wa ‘nguvu ya jina’ na kifuatacho ndicho anachokiamini, ‘ili ufanikiwe katika biashara ni lazima utengeneze jina na kamwe usiliharibu. Nguvu kubwa ya kiushindani niliyokuwa nayo wakati nilipoingia ubia katika biashara ya uzalishaji bidhaa ilikuwa ni jina langu “Dangote” ambalo nililijenga kwa juhudi kubwa katika kipindi changu chote nilichokuwa nafanya biashara ya uchuuzi wa bidhaa’.

Ukichukulia mifano ya makampuni makubwa kama Coca Cola, utakuta kuna wakati thamani ya jina huwa kubwa kushinda thamani halisi ya rasilimali yanazomiliki. Hiyo ndiyo nguvu ya kujenga jina zuri la kibiashara. Sasa kwa nini na wewe leo usianze kujijengea jina la kwako?

Ukweli ni kwamba jina lako la kibiashara laweza kuwa mwokozi wako katika nyakati ngumu kibiashara. Linaweza kugeuka nguvu kubwa ya kiushindani katika biashara yako ndogo.

3: UZA BEI NAFUU, ZINGATIA UBORA LAKINI ANGALIA USIUE USHINDANI

Katika kujenga biashara yenye mafanikio, Dangote anaamini kuwa umuhimu wa kuuza bidhaa bora katika bei nafuu. Kuuza bidhaa zilizo bora katika bei ambayo kila mteja ataimudu. Husaidia katika kuongeza utiifu wa wateja.

Kuhusiana na ushindani, Dangote anasema, ‘usiue ushindani, ndiyo afya kwa biashara. Unakuweka wewe mjasiriamali katika hali ya kuendelea kufanya jitihada zako zote ili kutimiza malengo’.

Mjasiriamali mwingine na aliyekuwa mwanaviwanda, Henry Ford wa Marekani, kwa upande wake aliwahi kusema, ‘kuna kanuni moja kwa mwanaviwanda, nayo ni kutengeneza bidhaa bora kabisa kwa kadiri inavyowezekana, katika bei nafuu kabisa inayowezekana huku ukilipa mshahara mkubwa kwa kadiri inavyowezekana’.

4: ANZA KIDOGO LAKINI UKIWA NA MAONO MAKUBWA

Kwa kuzingatia njia hiyo, Dangote anaeleza alivyofanikiwa, ‘niliunda makampuni na kuwa mtu mweusi tajiri zaidi duniani mwaka 2008.

Lakini hili halikuweza kutokea kwa siku moja. Ilinichukua miaka ipatayo 30 kufi kia hapa nilipo leo. Vijana wa leo wanatamani kuwa kama mimi lakini wanataka kufi kia lengo hilo kwa usiku mmoja. Hiyo haiwezi kufanya kazi. Kujenga biashara yenye mafanikio ni lazima uanze kidogo na kuota makubwa. Katika safari ya ujasiriamali, ung’ang’anifu katika kuyafi kia malengo ndiyo kila kitu’.

5: JENGA USHIRIKIANO, TAFUTA ‘MPENYO’ MKUBWA

Njia nyingine ya mafanikio ya Dangote ni ushirikiano kwenye biashara. Jamaa huyu anaheshimika kwa mtandao wake imara wa kibiashara pamoja na ushirikiano wa kisiasa. Unaweza ukajenga ushirikiano na kukuza mtandao wako wa kibiashara kwa kuongeza uwajibikaji kwa jamii, kuingia mikataba ya ubia, kuunda muungano wa kimkakati, kuhudhuria shughuli na mikutano ya kibiashara, kuchangia shughuli za kisiasa pamoja na kufanya ziara za kihisani.

Kudumu katika biashara ni lazima uimarishe ushirikiano wako kibiashara pamoja na mtandao na muhimu zaidi ni lazima uwinde ‘mpenyo’ mkubwa (big breakthrough). Mpenyo mkubwa ni muhimu mno katika uhai wa kijasiriamali. Ni vigumu mno kukuta mjasiriamali yeyote mwenye mafanikio ambaye hakupigwa jeki, kupitia mpenyo mkubwa.

Kwa mfano, Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alipata mpenyo wake mkubwa pale alipopata dili la kurekodi Wimbo wa Mbagala, hapo ndipo kila kitu kilipobadilika!

ITAENDELEA WIKI IJAYO.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply