The House of Favourite Newspapers
gunners X

Zitto Aanza Kujitetea Kesi ya Uchochezi – Video

0

MBUNGE wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameanza kujitetea katika kesi yake ya uchochezi inayomkabili kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo ameieleza mahakama kuwa, taarifa za mauji ya wananchi katika Kijiji cha Mpeta mkoani Kigoma alizipata kutoka kwa wananchi.

 

Akiongozwa na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, Zitto amedai kuwa taarifa nyingine alipata kupitia vyombo vya habari na kutoka kwa mmoja wa wabunge wa kigoma ambae alisema ndani ya bunge kuwa wananchi wake zaidi ya 20 wameuwawa na alitaka uchunguzi ufanyike.

 

Zitto amedai kuwa, maudhui yaliyokuwa kwenye kielelezo namba tatu ambayo ni taarifa aliyosoma kwa waandishi wa habari yalikua ni kutaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina wa masuala yaliyotokea Kijiji cha mpeta wilaya ya uvinza huku akiongezea kuwa lengo lake lilielezwa wazi kuwa baada ya uchunguzi hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote watakaobainika na mauaji ya wananchi.

 

Zitto amedai kuwa hakuna shahidi wa upande wa mashtaka aliyeleta nyaraka kuonyesha kuwa uchunguzi umefanyika na hakuna mtu aliyefariki. Zitto anatuhumiwa kwa makosa matatu ikiwemo kutoa maneno ya uchochezi anayodaiwa kuyatenda Oktoba 28, 2018.

 

Leave A Reply