The House of Favourite Newspapers
gunners X

Zitto: Bunge Liibane Serikali Kuhusu Mikopo – Video

MBUNGE wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amesema kuna umuhimu wa Bunge kuipangia serikali ya kiasi cha fedha inachotakiwa kukopa ili kupunguza kuongezeka kwa deni la taifa na mikopo husika itumike kikamilifu katika miradi ya maendeleo.

 

Alitoa kauli hiyo jana jioni Jumatano Juni 26, 2019 bungeni jijini Dodoma katika mjadala wa muswada wa sheria ya fedha mwaka 2019 unaotarajiwa kupitishwa leo Alhamisi Juni 27,2019.

 

“Mwaka huu tunatarajia kukopa Sh2.3 trilioni kama mikopo ya kibiashara lakini sasa hivi serikali inahangaika kutafuta mikopo ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

 

“Waziri wa fedha siku za hivi karibuni alikuwa Marekani na timu yake na walikutana na watu wa Benki ya Standard Chartered kuomba mkopo wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) wa Dola bilioni 1.5 kuanzia Morogoro mpaka Dodoma na kwenda mpaka Isaka,” alisema Zitto.

 

Alisema mkopo huo unaombwa lakini unakwenda katika ujenzi wa reli inayonufaisha nchi nyingine, si Tanzania.

 

“Ukitazama ukuaji wa bandari, bandari ya Kigoma inakua kuliko zote, mwaka jana imekua kwa asilimia 43.7 na inayofuata ni bandari ya Tanga, lakini bandari ya Mwanza ambako reli (ya kisasa) ndiyo inakoelekea kujengwa mwaka jana imekua kwa chini ya asilimia moja,” alisisitiza.

 

Duh! ZITTO ACHARUKA BUNGENI – “Tunaiua Tanzania, Ongozeni Sio Kutawala”

Comments are closed.