The House of Favourite Newspapers

Zitto: Serikali Ieneze Umeme Lakini Itunze Mazingira – Video

Mbunge wa Kigoma Mjini amesema hakuna mtu anayepinga Serikali kuongeza uwezo wa kuzalisha umeme lakini taratibu za kisheria na utunzwaji wa mazingira zifuatwe ili kuhakikisha nchi haiathiriki kwa ujumla wake kutokana na mradi mmoja ambao una mbadala wake katika Pori la Selous na Kilombero.

 

“Nikiangalia katika muktadha wa kiuchumi, nchi yetu tumepanga kufikia mwaka 2025 tuwe na watalii milion nane ambao watatuingizia zaidi ya dola bilioni 16 kwa mwaka. Hawa watakuwa wakitalii maeneo ya Ukanda wa Kusini na Magharibi na si Kaskazini kama ilivyo sasa, kama tutaondoa miti hii tutakuwa tunakinzana na mipango yetu.

 

Aidha, Zitto amesema iwapo jambo hilo litatekelezeka,  hata historia ya Spika Job Ndugai itafutika kwani aliwahi kufanya kazi pori la Selous, hivyo endapo litaondoka na historia yake haitakuwepo tena.

 

VIDEO: MSIKIE ZITTO AKIFUNGUKA

Comments are closed.