The House of Favourite Newspapers

Zitto kabwe Amtembelea Samatta Ubelgiji

MBUNGE wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemtembelea mchezaji wa Timu ya KRC Genk na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta nyumbani kwake Genk nchini Ubelgiji.

 

=========

ZITTO ANAANDIKA;

Nimepita Kumsabahi Nahodha Samatta

Jana jioni nilikwenda Genk, hapa Ubelgiji, nyumbani kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ndugu Mbwana Ally Samatta, ambaye ni mchezaji wa Klabu ya KRC GENK inayoshiriki Ligi Kuu ya hapa Ubelgiji.

 

Nimefurahi kupita kumsalimu na kumjua hali Samatta, nimefurahi zaidi kumkuta akiwa ni mzima wa afya na anashiriki mazoezi ya timu yake bila shida. Inatia moyo zaidi kuona Kijana huyu mwenzetu wa Kitanzania namna anavyofanya kazi kwa bidii ili aweze kufanikiwa zaidi.

Namuomba Mola amuwezeshe kutimiza ndoto zake.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo 
Genk 
Ubelgiji 
Februari 13, 2018

Comments are closed.