The House of Favourite Newspapers

Zitto Kabwe Asomewa Mashtaka Matatu Kisutu, Aachiwa kwa Dhamana

MBUNGE wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu -Dar leo Novemba 2, akitokea Kituo cha Polisi Mburahati ili kusomewa mashtaka yanayomkabili baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi na kukaa rumande tangu Oktoba 31, 2018.

Zitto anatuhumiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu mauaji ya baadhi ya askari polisi na wananchi katika kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza mkoa wa Kigoma ambapo baada ya kukamatwa alipelekwa kwenye Kituo cha polisi cha Oysterbay, kabla ya kuhamishiwa polisi kati na baadaye kulazwa kwenye kituo cha polisi Mburahati.

 

Kabla ya kukamatwa na Polisi, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno, alimtaka Zitto kuwasilisha alichokiita, “vielelezo vya madai yake,” kuwa watu zaidi ya 100 wameuwa katika eneo la Uvinza.

Zitto aliwaambia waandishi wa habari wiki iliyopita kuwa wananchi zaidi ya 100 wamepoteza maisha katika vurugu zilizoibuka kufuatia mgogoro wa ardhi wilayani Uvinza.

 

UPDATES:  ZITTO ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu – DSM, baada ya kusomewa mashtaka matatu yanayomkabili ikiwemo kutoa maneno ya uchochezi yenye nia ya kuleta chuki kwa Watanzania dhidi ya Jeshi la Polisi.

Amber Rutty, Mpenzi Wake, James Delicious Wafikishwa Mahakamani – Video

Comments are closed.