Ziyech Kumpisha Trossard Chelsea, AC Milan Yaonesha Nia Baada ya Kombe la Dunia
WINGA wa klabu ya Chelsea na Timu ya Taifa ya Morocco Hakim Ziyech huenda akatimka klabuni hapo na kuelekea katika viunga vya Estadio Guiseppe Meazza kujiunga na miamba ya soka nchini Italia, Klabu ya AC Milan katika majira ya dirisha dogo la mwezi Januari.
Taarifa kutoka katika vyombo mbalimbali vya Habari nchini Uingereza vimnebainisha kuwa tayari mabosi wa klabu ya Chelsea wameshaanza mazungumzo ya chinichini na wakala wa Leandro Trossard ili kuweza kutengeneza mazingira ya kukamilisha uhamisho wake wa kutimkia Darajani mwezi Januari.
Trossard na Ziyech wote watakwenda kuziwakilisha timu zao za taifa katika mashindano ya fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kufanyika nchini Qatar mnamo Novemba 21 mwaka huu.
Ikumbukwe Trossard ameshawahi kufundishwa na kocha mkuu wa sasa wa Chelsea Graham Potter wakiwa wote katika klabu ya Brighton and Hove Albion