The House of Favourite Newspapers

Zizzou Fashion yawapa vifaa vya michezo changanyikeni Rangers

0

,1Mkurugenzi wa duka la Zizzou Fashion, Athumani Tippo (kushoto), akimkabidhi vifaa vya michezo kocha wa timu ya Changanyikeni Rangers, Steven Nyenge, ndani ya duka hilo lililopo maeneo ya Sinza Afrika Sana jijini Dar es Salaam mapema leo.

44Tippo akiwa katika pozi na kocha wa timu ya Changanyikeni Rangers (katikati), na kocha wa timu ya watoto ya Boko Beach Veterani, Maswanya.

DUKA la vifaa vya michezo la Zizzou Fashion la jijini Dar es Salaam mapema leo lilijitolea kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu ya soka ya Changanyikeni Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Zizzou Fashion, Athumani Tippo, alisema amelazimika kutoa mchango wake kwa timu hiyo kutokana na kuonyesha juhudi, uwezo na kujituma kwa wachezaji wa timu hiyo kwa muda mfupi tangu ilipoanzishwa.

“Nimeamua kutoa mchango wangu wa vifaa vya michezo kwa timu hiyo kwani imenishawishi baada ya kuifuatilia kwa muda sasa ambapo nimeziona juhudi za kocha wao, Steven Nyenge, na wachezaji wote kwa jumla wanavyojituma kuhakikisha wanapanda daraja,” alisema Tippo.

NA MUSA MATEJA/GPL

Leave A Reply