The House of Favourite Newspapers

Zlatan: Messi Anajua Sana, ni Kama ‘Playstation’

 zlatann-and-messiLondon, England

STRAIKA mkongwe wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic ameuzungumzia uwezo wa soka wa Lionel Messi kwa kusema ni mchezaji wa kipekee na hakuna anayeweza kufanya yale anayoyafanya.

Ibrahimovic amezungumza hayo alipokuwa akizungumzia kikosi cha Barcelona alichocheza msimu wa 2009-10.

“Nafikiri Messi ni mchezaji wa kipekee, sijui kama tutaona mchezaji mwingine kama yeye, ana staili yake ya uchezaji, nilikuwa na bahati ya kucheza naye kila siku, ukimuona anacheza ni kama PlayStation.

“Ukimpa pasi anakuwa na uwezo mkubwa wa kuwapita watu. Wanazungumzia kuhusu kucheza ligi nyingine, mimi nimefanya hivyo na hata Messi angeweza kufanya hayo anayoyafanya popote pale.

“Anapenda soka wala hawezi kupata tabu kucheza kwa staili anayotaka akiwa nje ya Barcelona,” alisema Zlatan.

Aidha, Zlatan amewashauri Waargentina kujivunia kuwa na Messi kwa kuwa itawachukua miaka mingi kumpata mchezaji kama huyo.

Comments are closed.