The House of Favourite Newspapers

ZUBEDA: SIWEZI KURUDI KWA BARNABA NG’O!

Zubeda Namela

MZAZI mwenziye na mwanamuziki mahiri wa Bongo Fleva, Barnaba Elias ‘Barnaba Boy’ Zubeda Namela amefunguka kuwa kamwe hawezi kurudi kwa mzazi mwenziye huyo waliobahatika kupata mtoto mmoja kwa sababu kila mtu ana maisha yake mengine.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Zubeda alisema kila mtu kwa sasa yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaheshimiana katika hilo kilichobaki kwao kubaki kama wazazi na hakuna lingine zaidi ya hilo kwa sababu tangu wametengana ni muda mrefu sasa.

“Watu wanadai tu kuwa nimerudi kwa Barnaba, lakini sio kweli kabisa yule ni mzazi mwenzagu tu na ataendelea kuwa hivyo na si kitu kingine kwa sababu nina mtu wangu na yeye ana mtu wake kilichobaki ni heshima tu ya mzazi mwenzangu,” alisema Zubeda.

STORI: IMELDA MTEMA

Comments are closed.