Zuchu Aandika Historia Mlimani City, Apiga Shoo ya Kibabe – (Picha + Video)

SECOND lady kutoka lebo kubwa ya muziki Bongo, Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Zuhura Othman ‘Zuchu’ usiku wa kuamkia leo Februari 15, 2022 amefanya shoo yake maalum ya usiku wa Mahaba Ndi Ndi Ndi kwenye siku ya wapendanao katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Wasanii waliopafomu ni zaidi ya kumi wakiongozwa na, Zuchu baadhi yao ni staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Mbosso, Khadija Kopa, Mac Voice, Kassim Mganga, Malkia Patricia Hillary.
Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Mohamed Mchengerwa walikuwepo katika usiku huo.


