Kartra

Zuchu Afunguka Kutapeliwa

Mwanadada wa moto kunako Bongo Fleva, Zuchu kutoka Lebo ya Wasafi amefanya bidii kuwa kiasi cha kampuni kibao kumuona na kumpa madili ya ubalozi na matangazo.

Hata hivyo, inaonekana hajafurahishwa na baadhi ya kampuni anazofanyia kazi na huwenda akawa ametapeliwa kutokana na kile alichofunguka.

Kupitia Insta Story yake, Zuchu ameweka machapisho akiielezea kusikitishwa kwake na baadhi ya watu aliowafanyia kazi.

Ameandika; “Nimesikitika sana na baadhi ya watu ambao nafanya nao kazi, ifikie muda msanii aheshimiwa kwenye mitandao yake ya kijamii inayotumika kutangazia kitu f’lani.

“Hii siyo neema wala siyo msaada, tunafanya kazi kwa makubaliano, basi ifikie hatua mjifunze kuheshimu wasanii.”
Kama tunavyojua Zuchu huwa hatafuti kiki kwa mashabiki ili kibao chake kivume, lakini anasema kwamba wanawake wanapaswa kuheshimiwa.

“Na kinachokera zaidi ni kwamba unajua wanajua umefanya kazi kubwa kushikilia bango kwa kiasi kikubwa kuchangia ushawaishi kwenye matumizi ya kampuni zao.

“Watu wengi au makampuni wakati mwingine mna dharau sana wanawake kwenye upande wa malipo, heshimu mwanamke ambaye ametia bidii kwenye kazi yake. Nilipeni kile ninachodai siyo ombi…”
Je, ujumbe wa Zuchu unaendea kampuni gani? Au ni Wasafi?

Cc; @sifaelpaul


Toa comment