Zuchu Afungukia Kumng’oa Tanasha kwa Mondi

MITANDAONI kumewaka mbaya, watu wanasema ooh, staa mpya wa Bongo Fleva, Zuhura Kopa ‘Zuchu’ ndiye amehusika kwa kiasi kikubwa kumng’oa Tanasha Donna kwa mzazi mwenzake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, sasa basi, bibie huyo ameibuka na kufungukia madai hayo.

 

Madai ya mrembo huyo anayesumbua na ngoma ya Wana, yameibuka ikiwa ni siku chache tangu ajiunge na Kruu la Wasafi Classic Baby (WCB) na kupewa mapokezi kama yote na rais wa lebo hiyo, Diamond Platnumz mwenyewe!

Fununu zilieleza kuwa, mbali na bata analopewa kama msanii mpya, lakini eti alianza ‘figisufigisu za kuchukua namba’ kitambo na akafanikiwa.

 

“Iko hivyo, Zuchu alianza harakati kitambo, watu wamekuja tu kumuona anasajiliwa Wasafi, kumbe mwenzao alianza kitambo,” sehemu ya komenti za wambea wengi mitandaoni ilisomeka hivyo.

 

Akizungumza na WIKIENDA kuhusu madai hayo, Zuchu alisema hakuna watu anaowaheshimu kwenye muziki wake kama Diamond na familia yake yote kwa sababu ni watu ambao wamemfanya kuwepo mpaka sasa hivi alipo, lakini anashangaa sana kuona watu wameanza kumpaka matope kwa skendo hiyo ya Tanasha.

 

“Nilivyofundishwa sana hata na mama yangu, watu wa mitandao wanaweza wakanipotosha sana kwenye ndoto zangu, hivyo nisichukulie kila kinachosemwa kwa sababu kila mtu anaweza kuongea anavyotaka, sijahusika lolote na Tanasha, mimi nipo Wasafi kwa ajili ya kazi tu,” alisema Zuchu.

 

Mwanamuziki huyo aliongeza kuwa ameingia kwenye muziki akiwa ana imani ya kutimiza ndoto yake ya muda mrefu na pia anaheshimu sana mahusiano ya kila mtu na pia yeye bado binti mdogo hana muda wa kufanya yote hayo.

 

“Naheshimu mahusiano yangu mno, nahitaji sana kufikisha ndoto zangu mbele, ila sitawapa muda watu ambao wanataka kunivunja moyo, kikubwa nawaheshimu viongozi wangu wote wa WCB, kingine namheshimu sana Tanasha na kaka Diamond,” alisema Zuchu.

 

Mondi na Tanasha walimwagana mapema mwaka huu ambapo kabla ya kumwagana, walikuwa na ndoto za kufunga ndoa ambazo ziliishia njiani.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

 

 

 


Loading...

Toa comment