The House of Favourite Newspapers

Zuchu wa Mondi Hakamatiki

0

DAR: Hakamatiki! Kichwa kipya kwenye Bongo Fleva kutoka ndani ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura KopaZuchu’ anazidi kufanya vizuri tangu atambulishwe rasmi kama msanii wa lebo hiyo kubwa ya muziki nchini Tanzania kutokana na kufanya vizuri.

 

Katika rekodi mpya, Zuchu ameingia kwenye kumi bora ya wasanii waliotazamwa zaidi kwenye Mtandao wa YouTube kwa mwezi Aprili, mwaka huu kutokana na ubora wa kazi zake. Zuchu anashika namba ya sita akiwa ametazamwa na jumla ya watazamaji milioni 7.6.

 

Katika orodha hiyo, bosi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anaongoza kwa kutazamwa mara milioni 40.3. Staa mwingine mwengine wa lebo hiyo, Raymond Mwakyusa ‘Rayvany’ anafuatia nafasi ya pili akiwa na watazamaji milioni 17.8.

 

Namba tatu imekwenda kwa Rajab Abdul ‘Harmonize’ akiwa ametazamwa mara milioni 16.3. Hii ni ishara kuwa, spidi ya Zuchu ni ya ajabu hivyo kutishia kukalia kiti cha umalkia wa Bongo Fleva.

STORI: IMELDA MTEMA, Ijumaa

Leave A Reply