The House of Favourite Newspapers

Anayedaiwa Kuingiza Sh. Milioni 7 kwa Dakika Kizimbani

1

Kigogo Dakika 7

Mtuhumiwa Mohamed Yusuph Ally anayedaiwa kuingiza milioni 7 kwa dakika akipelekwa rumande.

MFANYABIASHARA anayedaiwa kukwepa kodi na kuingiza shilingi milioni 7 kwa dakika amesomewa mashitaka 199 leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kisha kupelekwa rumande.

4

Watuhumiwa hao wakipelekwa rumande.

Mtuhumiwa huyo aitwaye Mohamed Yusuf Ally alisomewa mashitaka hayo likiwemo la kugushi na kuwasilisha taarifa za uongo kwa kamishna wa TRA akidaiwa fedha zaidi ya shilingi bilioni 15 za Kitanzania.

5

Watuhumiwa wakitolewa eneo la mahakama.

Mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake watatu  hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi.

Hakimu aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, Huruma Shaidi aliiahirisha na akasema itatajwa tena Julai 25 mwaka huu

Habari na picha: Denis Mtima

CHEKI VIDEO HAPA

Video ya Dakika: Kamanda Sirro athibitisha kukamatwa kwa Gwajima

Police Wakamata Mashine za Kutengenezea Nyaraka za Serikali

1 Comment
  1. annie says

    HESHIMA YA NCHI LAZIMA IRUDI, HONGERA BABA RAIS

Leave A Reply