The House of Favourite Newspapers

Mshindi wa Nyumba ni Nelly Mwangosi wa Iringa

0

NYUMBA (1)

Meya wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Chaurembo akisoma jina la mshindi wa nyumba, ambaye ni Nelly Mwangosi kutoka Iringa.

https://www.youtube.com/watch?v=63utCkhhHso

NYUMBA (4)

MC Chaku akimpigia simu mshindi wa nyumba, Nelly Mwangosi kutoka Iringa.
NYUMBA (12)

Meya wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Chaurembo akizibwa macho ili akachague kuponi ya mshindi.

NYUMBA (13)

Abdallah Chaurembo akiwa na kuponi ya mshindi wa nyumba.

NYUMBA (7)

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akiwashukuru Watanzania wote walioshiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

Sweetbert Lukonge na Richard Bukos, DAR

HATIMAYE ile safari ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba iliyoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers, jana Alhamisi ilifika tamati baada ya kudumu kwa takribani miezi sita, ambapo kulifanyika kwa droo kubwa katika Viwanja wa Zakhem, Mbagala jijini Dar na mshindi kupatikana.

IMG_4926
Kuponi zote za nchi nzima zikimwagwa sehemu moja ili kumpata mshindi wa nyumba.

Nelly Mwangosi mkazi wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni mama wa nyumbani mwenye watoto wawili ndiye aliibuka mshindi wa nyumba hiyo ya kisasa iliyopo Salasala jijini Dar yenye samani zote za ndani mpya kabisa na mshindi huyo anatarajia kukabidhiwa mali yake hivi karibuni.

IMG_4912

Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers, Oscar Ndauka akichukua zawadi ya Dinner Set tayari kumkabidhi mshindi.

Mara baada ya kupigiwa simu kutaarifiwa kuwa yeye ndiye mshindi, mama huyo alisema “Yesu wangu!! Nimefurahi kuona kuwa nimeibuka mshindi, najisikia raha sana, nawaombea Global kwa Mwenyezi Mungu.” Shughuli hiyo ilitarajiwa kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye hata hivyo aliwakilishwa na Meya wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Chaurembo ambaye ndiye aliyesoma jina la mshindi huyo.

Bahati nasibu hiyo ya Shinda Nyumba ilisimamiwa na Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
IMG_4881

Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo akimkabidhi Peter Mihayo zawadi ya Bedsheet.

Mbali na mshindi wa nyumba, pia kulikuwa na zawadi ndogondogo zilizotolewa kwa washindi wengine. Washindi hao ni Peter Mihayo, Issa Leon Mallya, Frank Ndambo (wote Bed sheets), Mahmoud Mhina alishinda vyombo vya nyumbani (Dinner set) huku Method Kunambi na Halima wakishinda simu ya kisasa (Smartphone).
IMG_4922

Mahmoud Mhina akitokomea na zawadi yake ya Dinner Set.

Wengine ni ving’amuzi vitano vya TING ambapo washindi wake ni Godfrey Mkombo wa Morogoro, Wilbert John mkazi wa Kinondoni, Dar, Baltazar Mrosso kutoka Moshi, Magreth Ndambo wa Tabata, Dar sambamba na Jane Liwinga mkazi wa Dodoma. Pia Hawa Maulidi mkazi wa Mlole, Kigoma alishinda Bed Sheet, huku Helman Haule wa Dodoma akijinyakulia Dinner Set.

IMG_4910

Mmoja wa Ma MC wa kilele cha bahati nasibu ya Shinda Nyumba, Kelvin Shayo (kushoto) akiwa na mmoja wa wasomaji wa magazeti ya Global aliyekuwa akisoma jina la mshindi wa zawadi ya Bedsheet.

Bahati nasibu hiyo ya Shinda Nyumba ilikuwa ikiendeshwa na kampuni hii kupitia kwa magazeti yake ya Risasi, Amani, Uwazi, Championi, Ijumaa Wikienda yanayopatikana kwa shilingi 500 huku lile la Ijumaa linalotoka Ijumaa likiuzwa kwa shilingi 1,000 pekee.

IMG_4862

Burudani wakati wa kilele cha bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

Wakati mchakato wa kuelekea kumpata mshindi huyo jana ukiendelea, wananchi wengi walionekana kufurahishwa na kilichokuwa kikitokea huku wakisema kuwa Global imeweka historia kwa kuwa tukio kama hilo ni nadra kutokea kwa shilingi 500 kumpatia nyumba mtu tena ndani ya Dar es Salaam.
IMG_4907

Mshindi wa  simu ya kisasa (Smartphone), Method Kunambi (kulia) akipokea zawadi yake.

Aidha, kuna wale ambao walionekana kuwa na furaha kupitiliza na kujikuta wakitoa machozi ya furaha kwa kuona nyumba hiyo imeenda kwa mama wa nyumbani ambaye hana kazi. Katika maelezo yake Nelly alisema kwa sasa ana watoto wawili lakini alikuwa nao wanne, wawili walishatangulia mbele ya haki.

IMG_4879

Zoezi la kusoma majina ya washindi wa zawadi ndogondogo likiendelea.

Leave A Reply