The House of Favourite Newspapers

Mzee Yusuf: Wezi ‘Walinipiga’ Suti Sauzi

0

_MG_0017Mzee Yusufu.

Stori: Nyemo Chilongani, Risasi Jumamosi

Mfalme wa Muziki wa Taarab anayetamba na Wimbo wa Mashallah, Mzee Yusufu amefunguka kwamba ile suti nyekundu aliyoivaa katika video ya wimbo huo, aliibiwa Afrika Kusini alipofanya video ya wimbo huo.

Akizungumza hayo na mwandishi wetu, Mzee Yusufu alisema kwamba siku ya mwisho kufanya video ile aliamua kuiacha suti ile ndani ya gari ndogo aina ya Peugeot ambayo ilikuwa imekodiwa na wamiliki wa Studio ya Tupop Music Entertainment ila baada ya kumaliza video, walipokwenda sehemu ya maegesho gari hawakulikuta.

“Waliiba gari ambalo ndani yake kulikuwa na suti yangu nyekundu. Niliipenda sana, ilikuwa ni ya gharama kubwa ila ndiyo hivyo watoto wa Kisauzi wakaiba gari na suti hiyo. Iliniuma ila sikuwa na jinsi, niliamua kununua nyingine kama ile,” alisema Mzee Yusufu anayetamba na wimbo huo aliomshirikisha Vanessa Mdee.

 

Leave A Reply