The House of Favourite Newspapers

Wabunge 15 ‘visu’

6

site_197_Swahili_329474

Sifael Paul na Brighton Masalu

Upande wa pili! Bunge la 11 liliahirishwa Ijumaa iliyopita ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli aliwahutubia wabunge huku Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akihitimisha hotuba kwa kuliahirisha rasmi bunge hilo hadi Januari 26, mwakani.

Hata hivyo, hiyo siyo hoja wala gumzo kuu la bunge hilo ambalo linajumuisha wabunge wengi wapya kutoka vyama mbalimbali, lakini ‘pointi’ kubwa ni jinsi wabunge 15 wanawake ambao walilitikisa bunge hilo kutokana na urembo wao na kuzua gumzo kubwa.

Wabunge hao warembo a.k.a visu ambao umri wao bado ni ‘asubuhi’, walikuwa kivutio machoni mwa baadhi ya wabunge hususan vijana ambao ‘walivunjika’ shingo juu ya wawakilishi hao.

Ijumaa Wikienda linakupa orodha ya wabunge hao warembo ambapo waliojulikana kwa kukimbiza kama akina Halima Mdee wametakiwa kukaa chonjo. Hata hivyo, wabunge warembo wa kike ni wengi, lakini wafuatao ndiyo ‘shida’ kuanzia maumbo na sura zao.

magigeCATHERINE MAGIGE (CCM)

Rekodi ya urembo wake haijawahi kuvunjwa bungeni. Mara zote, tangu alipotinga bungeni mwaka 2010, amekuwa gumzo kubwa kwa uzuri wake, licha ya kushindanishwa na wabunge kadhaa, lakini bado ‘anatusua’ vilivyo.

BonnahBONNAH KALUWA (CCM)

Hii ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni. Uzuri na urembo wake umeonekana gumzo bungeni tangu mwanzo hadi mwisho wa kikao hicho. Sura, umbo na macho yake vimekuwa kivutio kikubwa.

kairukiANGELLA KAIRUKI (CCM)

Ukimwangalia vibaya, unaweza kusema ni shombeshombe. Urembo wa sura yake, umekuwa ukiwapa nyakati ngumu watu wengi, wakati mwingine kushindwa hata kung’amua kama ana asili ya Kiarabu au la! Kinachomuongezea sifa katika kilinge cha urembo ni umbo lake lililojengeka.

ESTER MATIKOESTER MATIKO (CHADEMA)

Achana na ukali wa hoja zake anapochangia mijadala. Hiki ni ‘kisu’ kikali kinachovutia bungeni. Umbo lake la ‘kitoto’, uzuri wa sura na macho ya mviringo, vinamfanya aonekane mrembo na mwenye uzuri wa kupindukia.
bukwimbaLOLESIA BUKWIMBA (CCM)

Tabasamu lake ndiyo limekuwa gumzo. Sura yenye uchangamfu imekuwa ikiteka macho ya watu wengi. Kamwe huwezi kuchoka kumtazama mwakilishi huyo. Mpole kama alivyo, lakini amekuwa ‘akikimbiza’ vilivyo mjengoni.

DK MARRY MWANJELWA (CCM)

Licha ya umri kuanza kumpigia honi lakini anawafunika wabunge wengi wenye umri mdogo. Urefu na figa nzuri, vinachangia kwa kiasi kikubwa kumweka kwenye orodha ya wabunge wa kike wanaotikisa kwa uzuri.

UMMY MWALIMU (CCM)

Hana makuu. Mpole na mwenye aibu wakati wote, lakini urembo wake unashereheshwa na umbo lake matata. Ana urembo wa haja unaoyapa macho kazi ya ziada kuitafuta kasoro yake.

CECILIA PARESSO (CHADEMA)

Urembo, uzuri wa umbo lake, urefu, unene wa wastani na sura nzuri vinatosha kumuingiza kwenye orodha hii.

shonza

JULIANA SHONZA (CCM)

Umbo lake ni la kawaida, lakini shughuli iko usoni. Achana na sehemu zingine za mwili, ukimtazama usoni tu utagundua ni kisu.

lucyLUCY MAYENGA (CCM)

Ni mrembo wa umbo na sura. Hahitaji maneno mengi kumwelezea, lakini ukweli unabaki palepale kuwa ni miongoni mwa wabunge warembo walioupa shida Mji wa Dodoma.

Mboni-MhitaMBONI MHITA (CCM)

Akiwa umbali kidogo kutoka mahali ulipo, unaweza kumchukulia kawaida! Shughuli ipo akikusogelea. Umbo na uzuri wake ni habari nyingine.

NEEMA MGAYA (CCM)

Rangi yake ya asili, ngozi laini, umbo namba nane na ucheshi wake, vinamtetea kuingia kwenye ulingo wa wabunge hawa warembo zaidi.

VICKY KAMATA (CCM)

Silaha kubwa aliyonayo ni midomo na macho! Geuza gazeti nyuma, mtazame tena Vicky, unaona? Si umbo, si sura, si macho, si mdomo, Vicky Kamata ni mrembo. Inatosha kusema hivyo tu.

JESCA KISHOA (CHADEMA)

Ni mrembo anayevutia kwenye viunga vya bungeni na inawezekana ndiyo maana aliyekuwa Mbunge wa NCCR-Mageuzi, David Kafulila aliamua kuchukua jumla na kumweka ndani.

bulayaESTER BULAYA (CHADEMA)

Kama unahitaji kumpongeza muumba kwa kazi njema, wewe mtazame Ester Bulaya, si mrefu, si mfupi, si mweusi wala si mweupe. Yuko kati kwa kati. Akitembea, kama ni barabarani, jihadhari na vyombo vingine vya usafiri.

6 Comments
  1. jacqy says

    Unaweza kusoma lakini uwelewi wamekwambia wabunge 15 visu awajakwambia wabunge wa ccm Ester ni wa ccm.

  2. jacqy says

    Alafu ndio supervisor

  3. soud says

    HAWANA UZURI WOWOTE

  4. Sarah marjan says

    wengine niwakawaida bwana, umewapaishaaaaaa!!!!!!!!

  5. Donnie says

    Kama ‘ my wife’ nae angekuwa mbunge kumbe angewakimbiza woooteh!

  6. reuben says

    amazing

Leave A Reply