The House of Favourite Newspapers

Who is the father (Nani baba wa mtoto?)

1

MG_1256Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Idris Sultan.

Stori: Mwandishi Wetu, WIKIENDA
DAR ES SALAAM: Who is the father (nani baba mtoto?) Hilo ndilo swali ambalo bado linaendelea kufukuta kwa kasi ya ajabu kadiri siku zinavyoyoyoma huku kila mdau na shabiki wa mwigizaji mwenye mvuto wa kipekee Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akitaka kupata jibu sahihi baada ya mrembo huyo kudaiwa kunasa ujauzito miezi michache iliyopita na wahusika wawili kutajwa, Ijumaa Wikienda linazidi kukuhabarisha.

MBUNGE ALIANZA KUTAJWA
Taarifa za ujauzito wa Wema na mhusika wa kwanza kutajwa ambaye ni mbunge mwenye fedha za kutosha wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa mara ya kwanza zilianza kuripotiwa na gazeti ndugu na hili la Ijumaa, Desemba 25, mwaka jana.

Licha ya mbunge huyo ambaye jina tunalihifadhi kwa sasa kutofunguka moja kwa moja gazetini, taarifa kutoka kwa mtu wake wa karibu zilieleza kuwa mwanasiasa huyo alielezwa kuwa ujauzito ni wake na kuanza kuhudumia huku mshindi wa Big Brother Africa ‘Hot Shot’ 2014, Idris Sultan naye akihudumia akiamini ‘mzigo’ huo ni wake kwani Madam amemhakikishia mimba ni yake.

WEMA-LOVEHABARI MPYA
Wikiendi iliyopita, mtu huyo wa karibu na mwanasiasa huyo alipenyeza ubuyu kuwa, mbunge huyo ameibuka na kuzidi kusisitiza kuwa mimba ni yake kwani ilipatikana kipindi cha kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015 uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wakati mbunge huyo alipokuwa ‘amemtaiti’ Wema.

“Rafiki yangu (mbunge) anaamini mimba ni yake kwa sababu hiyo mimba ilipatikana kipindi cha kampeni. Wakati huo huyo Idris hakuweza kupewa nafasi hata ya kumsogelea Madam, mtoto wa kike alitaitiwa kwelikweli na jamaa (mbunge),” alisema rafiki huyo wa karibu na mbunge.

wema-na-idriss-instaVITA IMEPAMBA MOTO
Imeelezwa kuwa, baada ya taarifa za mbunge huyo kujitapa zilimfikia Idris ambaye naye alizidi kukomaa kuwa ‘mzigo’ ni mali yake na mbunge anajisumbua tu kuhudumia.
Alipotafutwa Idris kuhusu taarifa hiyo hakutaka kufunguka moja kwa moja zaidi ya kusema apewe muda, ataeleza kila kitu.

“Nipe kama wiki moja au mbili hivi nitafafanua zaidi hilo japo sioni swali la msingi hapo wakati ipo wazi. Wewe unafikiri mimi nina wasiwasi? Acha hizo,” alisema Idris na kukata simu.

DAKTARI ATHIBITISHA
Licha ya Wema kushindwa kutegua kitendawili cha nani mhusika wa mimba aliyonayo lakini taarifa za uhakika ambazo Ijumaa Wikienda inazo kutoka kwa daktari aliyempima, zinathibitisha mrembo huyo ana mimba ambayo ina zaidi ya miezi minne.
“Maadili hayaniruhusu kutoa siri ya mgonjwa lakini wewe jua tu kuwa Wema ana mimba ya zaidi ya miezi minne,” alisema daktari huyo huku akiomba hifadhi ya jina.

1 Comment
  1. […] mfupi baada ya Gazeti la Ijumaa Wikienda kutoka na stori yenye kichwa cha habari “Who is the father (Nani baba wa mtoto?)” likiwa ndilo swali ambalo kila mdau na shabiki wa staa Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ anataka […]

Leave A Reply