Meya Ubungo Awasilisha Mashtaka Dhidi ya Mkuu wa Mkoa

MSTAHIKI Meya wa Jimbo la Ubungo (Chadema) Mh. Boniface Jacob ameelezea mafanikio ya vielelezo vya mashtaka aliyopeleka  Tume ya Maadili kuhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  yenye jumla ya makosa matano.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam meya huyo amesema kuwa siku ya Machi 22 mwaka huu, alipeleka rasmi mashtaka ya kumshtaki kiongozi huyo kuhusu kughushi vyeti, kula  kiapo cha utii kwa rais, matumizi mabaya ya madaraka na kujipatia mali kwa njia zisizo sahihi.

Ameongeza kuwa  pamoja na mashtaka hayo, aliwasilisha vielelezo  vya majina yake, vyeti na wanafunzi aliosoma nao.

Aidha amesema kuwa  Tume ya Maadili imeonyesha mwanzo mzuri ambapo imetoa majibu ya barua iliyopelekewa  kuhusu malalamiko hayo  na kero za mkuu huyo wa mkoa.


Loading...

Toa comment