The House of Favourite Newspapers

Prisons Kuingia Kambini Ijumaa

1
Kilichokuwa kikosi cha timu ya Prisons.

PRISONS keshokutwa Ijumaa inatarajiwa kuingia kambini kwenye hosteli zilizopo kwenye Gereza la Ruanda kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha wa Prisons, Mohamed Abdul alisema zoezi la usajili limekamilika na sasa ni muda wa maandalizi kuelekea msimu mpya wa ligi kuu.

“Tupo kwenye maandalizi ya kambi, Mungu akitujalia tutaanza Agosti 4 ya mwezi huu ili tuweze kujiandaa vizuri kwa msimu huu,” alisema Mohamed.

Naye nahodha wa Prisons, Laulian Mpalile alisema michuano ya hisani ya kuchangia mfuko wa kudhibiti Ukimwi imewasaidia kujua kikosi chao kina upungufu gani.

Pia Prisons itashiriki michuano ya Ujirani Mwema inayotarajia kuanza leo Jumatano kwenye Uwanja wa John Mwakangale wilayani Kyela.

1 Comment
  1. […] makini kilicho karibu na staa huyo kililitonya Ijumaa Wikienda kuwa, katika ndoa ya Masanja kulikuwa na changamoto kubwa kwani chokochoko na masimango vilikuwa […]

Leave A Reply