The House of Favourite Newspapers

Hiki Ndicho Wanawake Wengi Wanachokosa Kwa Waume Zao

1

NI wiki nyingine ninapokukaribisha mpenzi msomaji wangu katika ukurasa huu mzuri. Leo ningependa tujadiliane kuhusu jambo hili ambalo kwa kiasi kikubwa linawahusu wanaume ingawa wanawake nao wanapaswa kuelewa hali halisi. Kama wewe ni mume, mchumba au upo kwenye mapenzi ya kudumu na mwanamke fulani, unaelewa mwanamke wako anahitaji nini kutoka kwako?

Tukiulizana swali hili harakaharaka, majibu ambayo wengi watayatoa, huenda kwa kiasi kikubwa yatakuwa yakifanana. Wengi wanaamini kwamba mahitaji ya msingi ya mwanamke ambaye yupo kwenye uhusiano, ni huduma za kila siku, ikiwemo chakula, mavazi, fedha na malazi pamoja na kutimiziwa haja zao za kimwili.

Wengine wanaamini kwamba hitaji kubwa la mwanamke, ni pesa, yaani wewe mpe pesa za kutosha atatulia na wewe. Wengine wanafikiria kwamba labda ukimjengea mwanamke nyumba, ukamnunulia gari au ukimsomesha, basi hapo unakuwa umemaliza kazi.

Hata hivyo, uchunguzi wa muda mrefu wa wataalamu wa masuala ya uhusiano, unatoa majibu tofauti kabisa na kile watu wengi wanachokielewa au wanachokiamini. Matokeo yake, wanawake wengi wanakuwa wanakosa kile ambacho ndicho hasa wanachokihitaji kwa wenzi wao ndiyo maana matukio ya usaliti yamekuwa yakiongezeka kila kukicha.

Mwanamke anahitaji nini kutoka kwa mwenzi wake?

Haya ni baadhi ya mambo ambayo wanaume wengi hawayajui:

MPE KIPAUMBELE

Ni ukweli ulio wazi kwamba wanawake wengi wanapenda kupewa kipaumbele katika mambo yote yanayowahusu waume zao hata kama hawana uwezo wa kusaidia chochote. Kwa mfano, mwanaume anataka kununua kiwanja au nyumba kwa ajili ya kuishi yeye, mkewe na familia (kama anayo). Ni jambo zuri kabisa analolifanya lakini mwanamke asiposhirikishwa akaja kugundua mwenyewe, atajisikia vibaya sana na huenda hata mapenzi kwa mumewe yakaanza kupungua kwa kudhani anadharauliwa.

 

Wanawake wengi wanapenda kushirikishwa katika kila jambo linalowahusu waume zao. Mshirikishe katika mambo madogo na makubwa hata kama unajua hawezi kuwa na msaada wowote. Ukimpa nafasi hiyo, atajiona kuwa na nafasi kubwa kwenye maisha yako na atazidi kukupenda.

MUUNGE MKONO

Mnapoamua kuishi pamoja, mnakuwa kama timu moja ambayo maisha yenu yanategemeana. Im
ekuwepo kasumba ya mfumo dume kwa kipindi kirefu, wanaume wengi wakiamini kwamba wanawake ni watu dhaifu ambao hawawezi kuwa na mchango wowote kwa familia zaidi ya kutunza nyumba na kulea watoto. Haya ni makosa makubwa wanayoyafanya wanaume.

Mkeo anapokuja na wazo kwako, muunge mkono na mtie nguvu ili aone kama anaweza kufanya mambo makubwa. Pale anapokwama mshike mkono na muonyeshe njia, iwe ni kwenye biashara, kwenye kazi au kwenye mambo yake binafsi au ya familia. Muunge mkono, hiyo itasaidia sana kumfanyaaone umuhimu wako na atazidi kukupenda.

MSIFIE MARA KWA MARA

Ni ukweli usiopingika kwamba kihaiba, wanawake ni watu wanaopenda sana kusifiwa, hasa na waume zao au watu Wanaume wengi huwa na tabia ya kuwasifia wenzi wao katika siku za mwanzo za uhusiano wao lakini wakishazoeana, huacha kabisa. Usiache mkeo akasifiwe barabarani wakati wewe ndiye mwenye wajibu wa kumsifia.

 

MSIKILIZE, MPENDE

Wanawake wengi wanapenda kusikilizwa hata kama wanachokizungumza hakina maana. Anaweza kuwa anakusimulia habari za mashoga zake, watoto wa jirani au kuhusu filamu au tamthiliya anayoipenda. Msikilize na changia mazungumzo yake kuonesha mpo pamoja, hiyo itamfanya azidi kukupenda zaidi na kujisikia amani akiwa na wewe.

Baadhi ya wanaume huwa na kawaida ya kuwakatisha mazungumzo wenzi wao kwa kuona hayana maana au kuwa bize na mambo mengine, kwa mfano kuchezea simu au kuangalia TV wakati wenzi wao wakiwaongelesha. Mwisho muonyeshe kwamba unampenda na mara kwa mara mtamkie kwamba unampenda.

Nakupenda ni neno dogo lakini lenye umuhimu mkubwa katika uhusiano wa watu wawili walioamua kuishi pamoja. Kubwa na muhimu zaidi, hakikisha unamridhisha muwapo faragha. Ukifanya hivyo, maumivu ya mapenzi utayasikia kwa wenzako tu. TUKUTANE WIKI IJAYO

Na: HASHIM AZIZ

INASIKITISHA! SIMULIZI ya MJANE ALIYEFUNGWA MIAKA 22 kwa KUKUTWA na NYAMA ya SWALA KWENYE NDOO…

1 Comment
  1. […] huo ulibaini, kuna baadhi ya wanaume za watu wanashawishiwa na wadada hao wa saluni na kujikuta wakifanya ngono ndani ya baadhi ya saluni ambazo […]

Leave A Reply