Wakazi wa Kijitonyama Dar waanza usafi maeneo yao
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kijitonyama Mpakani ‘B’ wakifanya usafi kwenye maeneo yao.
Zoezi la kukusanya uchafu likiendelea.
“Hapa ni usafi tu”, ndizo hisia zinazoonekana kutawala zoezi wakazi wa Kijitonyama kusafisha mazingira yao.
Mtaro uliojaa uchafu ukisafishwa.
WAKAZI wa eneo la Kijitonyama Mpakani ‘B’ jijini Dar es Salaam wemeungana na Watanzania wengine kufanya usafi katika mitaa inayozunguka maeneo yao.
Zoezi hilo ni mwendelezo wa kauli ya Rais Magufuli kuwataka wananchi kufanya usafi kwenye maeneo yao ili kuondokana na balaa la ugonjwa wa kipindupindu.
Kwa upande mwingine zoezi hilo linakuja kufuatia kufutwa shamra za sikukuu ya uhuru zilizokuwa zifanyike Desemba 9 mwaka huu ili watu waitumie siku hiyo kwa kufanya usafi kwenye maeneo yanayoonekana machafu.
(NA DENIS MTIMA/GPL)


Comments are closed.