×

Dwight Yorke Aomba Kibarua cha Ukocha Aston Villa

SYDNEY, AUSTRALIA - DECEMBER 10: Dwight Yorke speaks to the media during a press conference at Museum of Contemporary Art on December 10, 2012 in Sydney, Australia. Manchester United will play an A-League All-Stars match in Sydney on July 20, 2013. (Photo by Mark Kolbe/Getty Images)

Dwight Yorke.

MCHEZAJI wa zamani wa Aston Villa, Dwight Yorke ametangaza rasmi kuwa anahitaji kuwa kocha wa klabu hiyo.

Dwight mwenye umri wa miaka 44, hana uzoefu mkubwa katika kufundisha soka lakini anahisi elimu yake ya masuala ya mpira wa miguu na uzoefu wake hasa katika ligi za Uingereza vinamfanya aamani kuwa anauwezo wa kuifundisha Aston Villa.

Ikumbukwe kuwa Dwight aliwahi kuichezea Manchester United na kuwa miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri zaidi katika kutekeleza wajibu wao wawapo uwanjani, pia hakusita kueleza kuwa anambinu za aliyekuwa kocha wake, Sir Alex Ferguson hivyo atatumia mbinu hizo kuifikisha mbali zaidi Aston Villa.

‘Nawafahamu vizuri wachezaji, utamaduni na historia ya Aston Villa. lakini cha ziada naifahamu nauelewa mkubwa kuhusu ligi za Uingereza.’

‘Nitaomba hiyo kazi (kazi ya kuifundisha Villa) na nitafanya kama navyoongea sasa. Natumaini watanipa inavyu nizungumze nao.’ Alisema Dwight.