×

Gazeti la Championi latoa tiketi kwa mashabiki Yanga, Al Ahly

1

Mashabiki wa Timu ya Yanga wakisaidiwa kukata kuponi baada ya kununua Gazeti la Championi Jumamosi ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

2

Shabiki wa Yanga akiweka kuponi yake kwenye ndoo maalum.

3

Mashabiki wa Yanga wakijaza kuponi zao baada ya kununua Gazeti la Championi Jumamosi.

4

Ofisa Masoko wa Global Publishers,Yohana Mkanda (mwenye kofia) akimshuhudia mmoja wa wasomaji wa Gazeti la Championi Jumamosi akijaza kuponi yake.

5

Mashabiki wa Timu ya Yanga wakichangamkia kununua gazeti hilo kwa muuzaji wa magazeti ya Global (katikati).

6

Mmoja wa mashabiki hao akionekana akijaza kuponi yake.

7

…zoezi likiendelea la kujaza kuponi.

8

Mashabiki hao wakingojea kuchezeshwa droo kabla ya mtanange kuanza

9

Kuponi zikichanganywa ili kumpata mshindi wa tiketi ya kuingilia kwenye mechi hiyo.

10

Kuponi ikiokotwa baada ya kuchanganywa.

 

12

Jina la mshindi likisomwa kwa ajili ya kupata tiketi yake.

13.Baadhi ya washindi waliojinyakulia tiketi za kuingia katika mechi hiyo kutoka kushoto ni, Abdallah Said, Omary S.Omary na Abdalla Kitulike (mwenye jezi ya zambarau) kulia.

Baadhi ya washindi waliojinyakulia tiketi za kuingia katika mechi hiyo kutoka kushoto ni,  Abdallah Said, Omary S.Omary na Abdalla Kitulike (mwenye jezi ya zambarau) kulia.

14

Baadhi ya washindi wa droo ndogo wakiwa katika picha ya pamoja na Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda (katikati).

GAZETI la Championi Jumamosi kupitia Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba leo limetoa tiketi kwa mashabiki wa mpira unaoendelea kuchezwa kati ya Timu ya Simba na Al Ahly ya Misri  kwenye Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.

Mashabiki hao walijinyakulia tiketi hizo kupitia droo ndogondogo zilizokuwa zikichezeshwa nje ya uwanja huo ambapo kabla ya kuchezeshwa wasomaji wa Gazeti la Championi Jumamosi walinunua gazeti hilo na kukata kuponi ili kushiriki Bahati Nasibu hiyo.

Wakati mashabiki hao wakijinyakulia tiketi hizo, pia walijipatia zawadi nyingine zilizokuwa zikitolewa baada ya kuchezeshwa droo ndogondogo hizo kama vile, fulana na kofia.

HABARI/PICHA: DENIS MTIMA/GPL

Leave a Comment