×

Mama: Jada alibamizwa ukutani, akapoteza kumbukumbu

Makala: Gladness Mallya

MSANII maarufu wa filamu Tanzania, Gladness Steven ‘Jada’ hivi sasa hali yake ni mbaya, akiwa anaishi na mama yake mzazi nyumbani kwao, Temeke eneo la Pile, baada ya kufikwa na maswaibu akiwa kazini.

Kwa mujibu wa mama mzazi wa Jada, Mary Charles, Jada alikuwa lokesheni wakishuti filamu, lakini katika sehemu ambayo ilitakiwa msichana huyo ionekane anabamizwa ukutani na mpenzi wake baada ya kuzozana, ikafanyika kweli badala ya kuigiza.

 “Walikuwa wakicheza filamu inayoitwa Penzi Mahututi, Hemed Suleiman ‘PHD’ alitakiwa aonekane anambamiza ukutani Jada, akambamiza kweli hali iliyosababisha kudondoka na kupoteza fahamu kwa saa mbili,” anasema mama Jada.

“Baada ya kupoteza fahamu, walimpeleka hospitalini ambako alipatiwa matibabu na kutakiwa kupumzika wiki moja huku akipewa dawa ambapo alizitumia kwa siku tano lakini kichwa kikaendelea kumuuma sana.

“Siku kadhaa baadaye hali ilibadilika na kupoteza kumbukumbu mpaka sasa haelewi chochote, kutokana na tatizo hili Jacqueline Wolper alijitolea sh. 315,000, ambazo alienda kufanyiwa kipimo cha CT- Scan katika Hospitali ya TMJ, Dar.

“Uchunguzi ulionesha kuna mtikisiko ulitokea kichwani, ndiyo sababu kubwa ya kupoteza kumbukumbu, alipewa dawa mpaka sasa anazitumia huku nikiendelea kumwekea picha mbalimbali alizocheza ili akumbuke maana haelewi chochote, kwani hata mimi ananiuliza ni nani.

“Siwezi kumlaumu Hemed, hii ni ajali kama nyingine ila mpaka sasa sijamuona kuja hapa kumuona, namshukuru sana Wolper kwa msaada wake, pia muongozaji aliyekuwa naye lokesheni, Lamata kwa misaada yao mikubwa, wameonesha moyo kwa kweli,” alisema mama huyo.

MSIKIE HEMED

“Kuhusu kumu-hudumia  kila kitu kiko sawa hayo mengi-ne ni maneno ya watu tu.”

LAMATA ANASEMAJE?

Gazeti hili lilimtafuta muongozaji wa filamu, Leah Mwendamseke ‘Lamata’ aliyethibitisha kwamba ni kweli tukio hilo lilitokea lakini ni bahati mbaya.

“Siwezi kuongea sana, maana siko sawa na mgonjwa bado hajawa sawa, ilitokea bahati mbaya,” alisema Lamata.

RAIS WA SHIRI-KISHO JE?

Rais wa Shirikisho la filamu ‘TAFF’, Simon Mwaki-fwamba alipotafutwa ili kujua namna wataka-vyomsaidia msanii huyo, alisema hana taarifa za tukio hilo, lakini atalifu-atilia ili kujua namna ya kufanya.