SIKU chache baada ya kuvuja picha zikiwaonesha wakiwa kwenye mapozi ya mahaba niue, mwanamama ambaye ni mkali kunako Muziki wa Mduara, Snura Mushi ameamua kuweka wazi kuwa, hana mapenzi yoyote na msanii mwenzake huyo, Benard Paul ‘Ben Pol’.
Akichonga na Showbiz Xtra, Snura anayebamba na Ngoma ya Shindu alisema, yeye na Ben Pol ni marafiki wa kawaida tu na siku hiyo picha zinazozagaa walikuwa wote na wasanii wengine wakijiandaa kwa Tamasha la Fiesta 2016 ambalo lilifanyika wiki iliyopita mkoani Singida.
“Sina uhusiano jamani na Ben, ukaribu wangu ni kikazi tu,” alisikika Snura.
Picha mbalimbali zimekuwa zikiwaonesha wawili hao wakiwa ‘very closed’ huku mashabiki wengi wakifurahia kwa kapo mpya mjini na wengine wakihoji ‘kupatwa kwa moyo mashine nini?’
Ben Pol na Snura katika picha ya kimahaba.