×

Makamu wa Rais Ahani Msiba wa Masaburi Leo

 msiba-wa-masaburi-1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha maombolezo  katika msiba wa marehemu Dk. Didas Masaburi mapema leo, Chanika jijini Dar es Salaam.

msiba-wa-masaburi-2

Akiwapa pole ndugu wa marehemu Dk. Didas Masaburi mapema leo Chanika jijini Dar es Salaam.

msiba-wa-masaburi-6 msiba-wa-masaburi-8

Akiendelea  kuwapa pole ndugu wa marehemu.

msiba-wa-masaburi-3

Wakiongea jambo.

msiba-wa-masaburi-9

msiba

Samia Suluhu Hassan akimpa pole na kumfariji Bi. Janeth Masaburi ambaye ni mke wa  Marehemu Dk. Didas Masaburi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amefika kuhani msiba wa marehemu Dk. Didas Masaburi, Chanika jijini Dar es Salaam ambapo pia amepata nafasi ya kumfariji mjane wa marehemu, Janeth.

Kwa mujibu wa msemaji wa familia hiyo, ambaye pia ni kaka wa marehemu, Otieno Igogo, mazishi yatafanyika Jumatatu.

Alisema mazishi yatafanyika eneo la Chanika kilipo Chuo cha Ununuzi na Ugavi (IPS), ambacho ni moja ya mali za marehemu kwa kuwa mwenyewe aliagiza azikwe kwenye eneo hilo.

Alisema marehemu enzi za uhai wake aliusia azikwe kwenye eneo hilo la chuo kwa kuwa ndipo alipoanzia maisha na watatimiza wosia huo.

Igogo alisema Dk. Masaburi alianza kuugua homa ya ini tangu mwaka 1997, lakini hali yake ilianza kuwa mbaya mwaka jana.
“Kutokana na kukubaliana kati ya familia na upande wa serikali, tumeamua azikwe hapa ili kutimiza alichokitaka tangu akiwa hai,” alisema Igogo.

WATOTO WA MAREHEMU
Watoto wa marehemu kwa nyakati tofauti walimwelezea baba yao jinsi alivyokuwa anawasisitiza kufuata maadili na namna walivyojitahidi kuwa naye katika matibabu.

Mmoja wa watoto hao, Agness Masaburi alisema alikuwa tayari kutoa sehemu ya ini lake ili kupandikiza kwa baba yake.
Alisema alisafiri pamoja na mama yake kwenda India katika hospitali zaidi ya nne kutafuta tiba.

Alisema mwanzoni mwa mwaka huu, walikwenda nchini humo katika Hospitali ya Safina kwa uchunguzi zaidi, kisha Hospitali ya Apollo, Global, HGS na Astery ambako madaktari walisema anaweza kutolewa sehemu ya ini na kupandikizwa jingine.

“Nilijitolea kama mtoto wake kutoa nusu ya ini langu, lakini mara ya mwisho tulivyokwenda Agosti mwaka huu, masharti yalikuwa nifikie uzito wa kilogramu 80 na mimi wakati huo nilikuwa na kilogramu 64,” alisema Agness.

Aliendelea kueleza kuwa baba yake pia aliambiwa apunguze uzito na kufikia kilogramu 100 au 90 kutoka kilogramu 151 alizokuwa nazo.

Agness alisema walipewa miezi mitatu kutimiza masharti hayo na walitarajia kurejea India Novemba mwaka huu kufanya upandikizaji huo.

Mtoto mwingine wa marehemu, Ojambi Masaburi, ambaye pia ni diwani wa kata ya Chanika, alisema baba yake alianza kusumbuliwa na ugonjwa huo Machi mwaka jana na aliwahi kulazwa katika Hospitali ya Regency jijini.

Alisema mwaka huu aliugua mara kwa mara na kumfanya asafiri zaidi ya mara tatu kwenda India kwa ajili ya matibabu.
“Alivyokwenda India Juni mwaka huu, alionekana ana uzito mkubwa wa kilogramu 151 kuna kipindi lakini alizipunguza hadi kufikia 124.
Alisema alifikishwa zahanati ya Ukonga usiku wiki iliyopita baada ya presha kushuka na ilipofika asubuhi alihamishiwa Regency kwa matibabu zaidi lakini hali haikuimarika.
Alisema Oktoba 2, alihamishiwa MNH kwa matibabu zaidi na lakini juzi majira ya saa 3:30 usiku akafariki.
Mtoto mkubwa wa marehemu, Steven Masaburi alisema kuwa baba yake alikuwa ni mtu wa watu, aliyependa kuzungumza na kila mtu.
“Baba alikuwa ni mtu wa watu, mcheshi, ambaye alitufundisha mema, aliwahi kutuambia kuwa itakapotokea akafariki, tumzike hapahapa chuoni,” alisema.
Kwa mujibu wa Igogo, Dk. Masaburi amefariki akiwa na umri wa miaka 56 na ameacha watoto 20 aliwapata akiwa na wanawake watatu. Alisema ana wajukuu wengi ambao idadi yake haikufahamika mara moja.

MAGUFULI AMLILIA
Rais John Magufuli jana alituma salamu za rambirambi kwa familia ya Dk. Masaburi kutokana na kifo kiongozi huyo wa zamani wa serikali.

Katika salamu hizo, Rais Magufuli alisema amepokea taarifa ya kifo cha Dk. Masaburi kwa mshituko na masikitiko na anaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao.

“Poleni sana familia ya Dk. Didas Masaburi, najua huu ni wakati mgumu sana kwenu, lakini niwahakikishie kuwa sote tumeguswa sana na msiba huu kwa kuwa tumempoteza mtu muhimu, msomi mzuri, kiongozi aliyelitumikia Taifa kwa moyo wake wote na aliyesimamia kile alichokiamini,” taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilieleza ikimnukuu Rais Magufuli.

Aidha, katika salamu hizo, Dk. Magufuli aliwapa pole wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wamempoteza mwanaCCM mwenzao pamoja na viongozi na watumishi wa jiji la Dar es Salaam ambao walifanya naye kazi alipokuwa meya.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Dk. Masaburi aliwania nafasi ya ubunge katika jimbo la Ubungo kupitia CCM, lakini akashindwa na Saed Kubenea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadem