×

Mahakama ya Ardhi Yatupilia Mbali Kesi ya Mbowe Hotels Ltd Dhidi ya NHC

1  

Wakili wa NHC, Aliko Mwamnenge akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka katika hukumu ya kesi hiyo.

2

Wakili wa Mbowe Hotels Ltd, John Mallya akizungumza na waandishi wa habari juu ya hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Ardhi.

3

Mawakili wakitoka mahakamani leo mara baada ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa.

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi imefuta kesi iliyofunguliwa na Mbowe Hotels Ltd dhidi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuwa Shirika hilo liliitoa kampuni hiyo katika jengo lake jijini Dar es salaam kwa kufuata taratibu zote na kuzishikilia mali zake kihalali.

Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Sivangilwa Mwangesi, ambaye amesema madai ya Mbowe kwamba aliingia mkataba na NHC hayana mashiko na kwamba mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.

Mlalamikaji alikuwa akidai kwamba wakati NHC inamtoa kwenye nyumba alikuwa ndani ya Mkataba wa Ubia na NHC, lakini Jaji alikataa hilo na kusema ingawa Mkataba wa Ubia ulikuwepo lakini haukutekelezwa ipasavyo.

Na wakati wa NHC kumtoa kwenye nyumba walikuwa na mahusiano ya mwenye nyumba na mpangaji, mahusiano ambayo yako wazi kisheria juu ya utekelezaji wake.

Naye wakili wa upande wa Mbowe Hotel Ltd, John Mallya amesema wamepokea hukumu na kuomba nakala ili kuweza kuifanyia kazi na kuongeza kuwa wakiipata nakala hiyo wanaweza kuamua iwapo wakate rufaa.