Basi la Hood Lagongana na Lori na Kupinduka Mlima Kitonga
Global Publishers October 28, 2016
SHARE THIS:
IRINGA: Basi la abiria ambalo ni mali ya Kampuni ya Hood linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Arusha jana mchana lilipata ajali na kupinduka katika Mlima Kitonga mkoani Iringa baada ya kugongana na lori la mafuta.
Imearifiwa kuwa, katika ajali hiyo mtu mmoja amepoteza maisha na wengine 43 wamejeruhiwa.
Kati ya majeruhi hao 25 wapo Hospitali ya Itunda Ilula na 18 wapo katika Hospitali ya Mkoa wakipatiwa matibabu.