Rais John Magufuli amemteua Jenerali Mstaafu George Waitara (pichani juu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza jana.
Rais John Magufuli akiwa na Jenerali Mstaafu George Waitara. (Picha na Maktaba)
Pia, Rais Magufuli amemteua Dk Eligy Shirima kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (Taliri)
Uteuzi wa Dk Shirima nao umeanza jana.
Kabla ya uteuzi huu Dk Shirima alikuwa Mtafiti Mkuu na Msimamizi wa Utafiti wa Nyama ya Ng’ombe Makao Makuu ya Taliri.
