Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi baada ya kuichapa mabao 3-0 timu ya Mbao FC kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyopigwa leo Uwanja wa Uhuru jijini Dar.
Kikosi cha Yanga SC.
Kikosi cha Mbao FC.
Patashika wakati wa mtanange huo.
Amisi Tambwe akikwaana na mabeki wa Mbao FC.
Simon Msuva (kulia) kazini.
Vicent Bossou akiruka kichwa langoni mwa Mbao FC.
Kikosi ya Yanga SC leo kimevuna pointi tatu baada ya kuichabanga Mbao FC kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga yamewekwa kimiani na Vicent Bossou katika dakika ya 49 akiunganisha kwa kichwa krosi safi iliyopigwa na Haruna Niyonzima. Bao la pili lilifungwa na Mbuyu Twite baada ya kurusha mpira uliokwenda moja kwa moja wavuni baada ya kipa kuupangulia ndani dakika ya 55.
Amisi Tambwe alihitimisha mabao kwa kuweka kimiani bao la tatu dakika ya 75 akiunganisha pasi ya Simon Msuva na kufanya matokeo kuwa 3-0 hadi dakika 90 za mchezo.
PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL







