×

Twanga Walivyonogesha Mambo Ndani ya Mango Garden

BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, usiku wa kuamkia jana Jumapili ilifanya onesho ndani ya Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar, sambamba na mkali wa muziki wa singeli maarufu kwa jina la Sholo Mwamba.

Katika onesho hilo mambo kadhaa ya kiburudani yalijili. Angalia picha.

twanga-pepeta-1 Khalid Chokoraa na Otilia Boniface wakicheza kimanjonjo sambamba na wanenguaji wengine.

twanga-pepeta-2Miraj Shakashia ‘Shakazulu’ akichagiza kwa gitaa.

twanga-pepeta-3Wanenguaji wa kiume kazini.

twanga-pepeta-4Mashabiki hawa wakifanya nao mmh!

twanga-pepeta-5Rapa Saulo John ‘Ferguson’ (kushoto) na muimbaji Kalala Junior wakinogesha mambo.

twanga-pepeta-6Pedeshee, Rehema Kiluvia akiwatunza wanenguaji.

twanga-pepeta-7Mkaza vitanda maarufu Dar, akiserebuka sambamba na manenguaji wa Twanga.

twanga-pepeta-8Sehemu ya mashabiki wakifutilia burudani.

twanga-pepeta-9Wanenguaji wa Twanga waliokuwa wakipiga mzigo Uarabuni kwa muda, Hamida (kushoto) na Fasha Joshua wakionesha mavitu ya Uarabubuni baada ya kurejea.

twanga-pepeta-10Mama Wema, Bi Mariam Sepetu nae alikuwepo kwenye onesho hilo, hapa akiwapa zawadi wadada walipendeza na vazi la kijora.

twanga-pepeta-11Mdada aliyependeza na vazi la kijora.

twanga-pepeta-12Asha Baraka akitangaza siku ya kuzaliwa ya mmoja wa mashabiki wa bendi hiyo ambaye alikuja na keki iliyoliwa ukumbini hapo.

twanga-pepeta-13Dada Asha Baraka (kushoto) na Mama Wema wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati mambo yakiendelea.

HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL