IKIWA ni miaka 20 tangu kifo cha aliyekuwa rapa mkongwe, Tupac ambaye mpaka sasa bado yumo kwenye mioyo ya wapenzi wa hip hop na mashabiki wa muziki, barua ambayo aliiandika, mwenyewe staa huyo wakati akiwa gerezani huko New York’s Clinton Correctional Facility mwaka 1995 inatarajiwa kuuzwa kwa kiasi cha dola za Kimarekani 172,750 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 378 za Kitanzania.
Taarifa iliyotolewa na Ken Goldin ambaye ni mwanzilishi wa Kampuni ya Goldin Auctions inayojihusisha na biashara za mauzo mitandaoni, imesema barua hiyo iliyondikwa na Tupac Shakur ni moja ya vitu kumi vilivyokuwa vikimilikiwa na rapper huyo ambavyo vyote vitauzwa kwa mtonyo wa $206,625.
Barua hiyo yenye kurasa nne ina kichwa cha habari “Is Thug Life Dead?” mwanzoni ilikuwa ikiuzwa kwa thamani ya dola $225,000 na mfanyakazi wa kampuni ya Death Row Records, Nina Bhadreshwar, aliifungua kwa mara ya kwanza Mei 6, 1995.
Pac alipelekwa jela baada ya kushtakiwa kwa tuhuma za udharirishaji wa kijinsia ambapo alikana shtaka hilo na miezi mitatu baadaye aliandika barua hiyo.
Baadhi ya maneno yaliyomo kwenye barua hiyo;
“I did not begin thug life,” ‘Pac writes in the letter. “I just personified it. I couldn’t stop it if I tried but in my heart the thug ni**a has advanced 2 be a Boss Playa. So No Thug Life is Not Dead but in my heart it is. If U are sharp u will learn from this.” Ameandika Pac.