Michuano ya Ligi ya Europa iliendelea jana usiku, November 3 kwa michezo kadhaa kupigwa huku Manchester United ikiendelea kupoteza michezo yache baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa wenyeji wao Fenerbahçe.
Kocha wa Man U, Jose Mourinho amewaangushia lawama wachezajiwake kwa kukubali kichapo hicho dhidi ya Fenerbahce huko Istanbul.
Mourinho kwa upande wake alianza kupoteza matumaini ya mechi hiyo kunako dakika ya 65 kwenye Uwanja wa Sukru Saracoglu Stadium licha ya bao la Wayne Rooney la 38 kwenye michuano ya Europea akiifikia rekodi ya Ruud van Nistelrooy.













