×

Mercy Johnson ni Mwathirika wa Ubaguzi wa Rangi Nollywood

mercy-johnson-december-2013-bellanaija-04NIGERIA: Mwigizaji maarufu wa filamu nchini Nigeria (Nollywood), Mercy Johnson Okojie (32) ameanika namna ambavyo amekuwa akinyanyaswa naa baadhi ya waandaaji wa filamu nchini humo kutokana na kumnyima fursa ya kuigiza kwenye baadhi ya scene kwa kile wanachodai kuwa rangi ya ngozi yake ni nyeusi, hivyo hawezi kuwa na mvuto kwenye runinga kama walivyo wanawake weupe.

ajg_baby-henry-066Msanii huyo ambaye anafanya vyema kwenye tasnia hiyo, ameeleza hayo alipokuwa akihojiwa na Televisheni ya Pulse kwenye kipindi maalum cha maisha binafsi ya wasanii nchini humo, huku akieleza kuwa amekuwa akikumbana na chngamoto nyingi kwenye fani yake ya uigizaji likiwemo swala la kunyimwa fursa ya kuigiza kwa madai kwamba ngozi yake nyeusi haiuzi runingani.

mercy-johnson-december-2013-bellanaija-012Ameeleza kuwa, waandaaji wa filamu waliyo wengi hupenda kufanya kazi na mabinti wenye ngozi nyeupe na laini wakifikiri kuwa hao ndiyo wenye vipaji, kumbe ngozi nyeusi ndiyo yenyewe iliyobeba vipaji.

Jambo hilo limekuwa likimkera licha ya yeye kutokata tamaa na kuendelea kupambana zaidi ili afikie malengo yake.

Maneno yake:    image-58

Mercy hajasita kueleza pia kuwa huenda hiyo ndiyo sababu ya wasichana na wanawake wengi nchini nigeria kujichubua ngozi zao nyeusi ili wawe na ngozi nyeupe.