×

Mgonja: Watumiaji Wa Barabara Kupatiwa Elimu Wiki Ya Usalama Barabarani

1

DAR ES SALAAM: MWENYEKITI wa Kamati ya Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam,  Elifadhili Mgonja (pichani anayezungumza) amesema kuwa watumiaji wa barabara za Mkoa wa Dar es Salaam, watapatiwa mafunzo na elimu juu ya matumizi sahihi katika kuendesha vyombo vya moto barabarani.

2…. Akionyesha stika za magari na pikipiki watakazozitoa siku hiyo.

Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yanayotarajiwa kufanyika Novemba 7 mwaka huu kwenye viwanja vya Temeke- Mwembe Yanga Dar.

3

Mratibu Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Peter Mashishanga (katikati) akifafanua jambo.

Amesema kuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda huku shughuli mbalimbali zikifanyika siku hiyo ikiwemo ukaguzi wa magari na kupatiwa stika maalum endapo vyombo hivyo vitakuwa vimethibitishwa kutembea barabarani.

4Meneja uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele naye akizungumza jambo.

Aidha Mgonja alisema kuwa wiki ya nenda kwa usalama barabarani hufanyika kila mwaka nchini kote na maadhimisho hayo kitaifa yalifanyika mkoani Geita Septemba 26 mwaka huu.

“Maudhui ya maadhimisho haya ni kutathmini hali ya usalama barabarani na kutoa  elimu ya usalama barabarani kwa watumiaji  wote wa barabara,” alisema.

5Meneja uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni tanoMwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam,  Elifadhili Mgonja (kushoto).

Naye Meneja uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele amesema wameamua kuunga mkono maadhimisho hayo siku hiyo ili kuhakikisha usalama wa raia unakuwa salama katika kujenga uchumi wa nchi.

6-wanahabari-wakichukua-tukio-hiloWanahabari wakichukua tukio hilo.

Amesema PPF wameamua kuunga mkono kwa kukabidhi hundi ya Sh. Milioni tano ili kuweza kufanikisha shughuli hiyo.

Na Denis Mtima/Gpl