×

Shigongo Atoa Vitabu 20 Kwa Washindi

kitabu-1Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kulia) akimkabidhi zawadi ya kitabu Selina Ezekiel katika Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar leo.

kitabu-2

Teddy Andrew (kushoto) akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.

kitabu-3

Magreth Mgina (kushoto) akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.

kitabu-4Ngoshilendi Mpatu (kushoto) akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.

kitabu-5Elinath Hillary (kushoto) akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.

kitabu-6Washindi wakiwa katika picha ya pamoja.

kitabu-8

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo akizungumza na washindi hao.

kitabu-9…Akiendelea kuongea nao.kitabu-10 kitabu-11 kitabu-12 kitabu-13Washindi wakiwa katika pozi tofauti na Eric Shigongo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo ametoa zawadi ya vitabu vya hadithi ya Rais Anampenda Mke Wangu na Jinsi ya Kutoka Umasikini Hadi Mafanikio kwa washindi watano ambao walishiriki katika kushare page yake ya Facebook ijulikanayo kama Eric Shigongo.

Tukio hilo la kutoa zawadi limefanyika leo hii katika Ofisi za Global Publishers, kampuni inayotengeneza Magazeti ya Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani na Championi, zilikabidhiwa kwa washindi hao na Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho.

Mbali na washindi hao kupokea zawadi hizo, pia walipata nafasi ya kuzungumza na Shigongo ambaye amewataka kuendelea kufuatilia page yake ambayo inaandika zaidi kuhusu mambo ya ujasiriamali na hadithi zake mbalimbali.

“Kwanza nashukuru kwa mchango wenu, ninaona kila kitu kinachoendelea na ninafurahi kuona familia yetu ikiendelea kuwa kubwa. Msichoke kushare kile kinachowekwa. Peke yangu siwezi, ninatamani nimfikie mmojammoja lakini nashindwa kutokana na wingi wenu. Ila kwa kile mnachokifanya, ninawashukuru sana,” alisema Shigongo wakati alipokuwa akizungumza na washindi hao.

Mbali na washindi hao ambao wamekabidhiwa vitabu hivyo, pia vitabu vingine vitatarajiwa kutolewa kwa washindi ishirini waliokuwa katika mikoa mbalimbali hapa Tanzania. 

Unataka kushiriki? Unaweza kutembelea Page ya Eric Shigongo katika Mtandao wa Kijamii wa Facebook au ingia www.facebook.com/shigongotz