×

Cristiano Ronaldo Aongeza Mkataba Madrid Hadi 2021, Anyakua Tuzo LaLiga

cristiano ronaldoMadrid, Hispania: Straika wa Klabu ya Real Madrid na nahodha wa Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amekubali kuongeza mkataba mpya utakaombakiza klabuni hapo kwa miaka mitano June 2021.

ronaldoNyota huyo wa dunia mwenye umri wa miaka 31, mkataba wake wa sasa unamalizika June 2018 lakini Ronaldo amesaini  mkataba mpya jana Jumatatu ambapo ataendelea kulipwa mshahara wake wa awali wa Euro 365,000 kwa wiki.

cristiano-ronaldo-aongeza-mkataba-madrid-hadi-2021-2 Ronaldo akinyakua Tuzo ya Mchezaji Bora wa LaLiga

CR7 ambaye jana alishinda tuzo ya Marca’s Alfredo di Stefano, ameshafunga magoli 371 tangu alipojiunga na Madrid akitokea Manchester United mwaka 2009 huku akifunga magori 35 na kutoa assists 11 kwa msimu wa LaLiga uliopita huku akiisaidia timu yake ya Taifa ya Ureno kushinda Kombe la Uefa Euro 2016 kwa kuipiga Ufaransa bao 1-0 kwenye mechi ya fainali.

atleticoMlinda Mlango wa Atletico Madrid, Jan Oblak alitunukiwa tuzo ya Zamora kama kipa aliyezuia magoli mengi zaidi.

Pia ameisaidia Madrid kushinda taji la Champions League mara mbili taji moja la La Liga tangu alipohamia makao makuu ya Hispania miaka saba iliyopita.

diego-simeoneBosi wa Atletico Madrid, Diego Simeone alipata Tuzo ya Miguel Munoz kama Kocha Bora wa Mwaka.

Real Madrid walitoa taarifa yao inayosema kwamba Ronaldo atasaini makataba mpya wa kusalia Bernabeu tangazo ambalo limekuja wiki moja baada ya mchezaji mwenzake Gareth Bale kuongeza mkataba hadi mwaka 2022 na miaka hiyo ya soka la Hispanaia.

suaresSuarez wa Barcelona alichukua Tuzo ya Pichichi ya Mfungaji Bora wa Mwaka wa LaLiga 2015-2016.

Ronaldo alikisaidia kikosi cha Madrid kupaa hadi nafasi ya kwanza La Liga baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Laganes siku ya Jumapili ambapo wameizidi Barcelona kwa pointi 2.

moratta Morata wa Real Madrid akipokea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Hispania wa Mwaka 2015-16

Baada ya mchezo, kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane alimsifia Ronaldo kwa kusema ni mchezaji wa kipekee.

Zidane aliongeza: “Ni ndo yake kumaliza maisha yake ya soka akiwa hapa.”

“Ninafuraha kwamba anaweza kuongeza mkataba na kumaliza soka lake akiwa anavaa jezi nyeupe kama nilivyofanya miaka mingi iliyopita.”