×

Rais Obama Amualika Donald Trump Ikulu Leo

trump-obamaRais Barack Obama wa Marekani  amempongeza Rais Mteule wa taifa hilo, Donald Trump na kumualika Ikulu kujadiliana juu makabidhiano ya ofisi.

obama-na-trump

Maelfu waandamana kupinga ushindi wa Trump

Kumekuwa na maandamano ya kupinga ushindi wa Donald Trump kutoka katika miji mbalimbali nchini Marekani.

Maelfu ya raia kwa sasa wamekusanyika nje ya mnara maarufu kama Trump Tower mjini New york wakipaza sauti zao kuhusu sera za uhamiaji,mapenzi ya jinsia moja na haki ya uzazi yanayopingwa na Donald Trump.

Wanasema hata dunia ina wasiwasi juu ya ushindi wa urais.