×

Baada ya Kupokonywa MTV EMA, Wizkid Kuzipotezea Tuzo za Muziki Kama Awali?

Wizkid1wizNIGERIA: IKUMBUKWE kuwa msanii wa Nigeria anayekimbiza na ngoma zake kali ikiwemo Ojuelegba, Wizkid siku za nyuma hakutaka kujishusisha na mambo ya Tuzo huku akiziponda hasa za MTV ambazo zilizokuwa zikitolewanchini Marekani ambapo wasanii wa Afrika hupewa tuzo hizo asubuhi na Wazungu wanapewa usiku.

hahaLakini siku za hivi karibuni baada ya kuibuka na ushindi wa kishindo kwenye Tuzo za MTV MAMA 2016, zilizofanyika hivi karibuni nchini Afrika Kusini, huenda aliamua kuufungua moyo wake.

alikibakitangomae1425110978813.jpgKiba

Inavyoonekana kwa sasa kuna kila dalili kwamba atarejea tena kwenye msimamo wake ule ule wa awali wa kuzichukulia tuzo kama si kitu cha maana baada ya MTV EMA kusitisha ushindi wake, kumnyang’anya tuzo hiyo na kumpa Alikiba kwakuwa ndiye aliyestahili kushinda kwa mujibu wa kura .

Mashabiki kibao wa Ali Kiba wamemnanga Wizkid kupitia akaunti yake ya Instagram huku wakimporomoshea maneno, mengine yakiwa yamejaa kejeli ambazo huenda kimemwongezea hasira zaidi alizozipata baada ya kupewa taarifa hiyo mbaya kiasi cha kuamua kufuta post alizokuwa ameweka kwenye Instagram kusherehekea ushindi wake huo.

Mbali na Instagram, katika akunti yake ya Twitter Wizkid ameponda vibaya watu wanaoandaa tuzo hizo kwa kuandika maneno makali bila ya kuwataja moja kwa moja jambo ambalo watu wengi wanadai huenda akazikacha kabisa tena tuzo hizo kama zamani.wizkid