×

Brazil Yainywesha Argentina Bao 3-0, Messi Hoi kwa Neymar!

brazil-cropped_8djocfwp0sqb1uypopdzxqebt-640x360Kujua anajua sana na uwezo wake ni wa tofauti na wengine. Akiwa na miaka 17-18 tu tayari alikuwa ngumzo nchini Brazil baada ya kuisaidia Klabu yake ya Santos kutwaa ubingwa wa Brazil mara mbili mfululizo pamoja na ule wa klabu bingwa barani America mara moja. Anafahamika kama Neymar Jr japo jina la kupewa na wazazi wake ni Neymar da Silva Santos Júnior .
 
neymar-messi-afp_806x605_51478835409Neymar ambaye mapema mwaka huu alikibwaga kitambaa cha unahodha wa kikosi cha Brazil ameendelea kuonesha uwezo wake wa kulibeba taifa pamoja na kuwa na umri mdogo. Katika rekodi zake za kuitumikia timu ya taifa, Neymar ameongeza rekodi nyingine baada ya kufikisha mabao 50 na kuwa mchezaji wa kwanza Barani Amerika ya Kusini mwenye umri mdogo zaidi kufikisha idadi hiyo ya mabao akiwa na umri wa miaka 24.
neymar-brazil-argentina-messi-wcq-1024x570
Bao moja alilofunga kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Argentina, limemfanya awakaribie wafungaji watatu wa muda wote wa Brazil ambao ni Romario mwenye mabao 50, Ronaldo de Lima mwenye mabao 62 na Mfalme wa soka duniani Pele mwenye mabao 77.Mbrazil huyo alikuwa kwenye kiwango kizuri mbele ya nyota mwezake wa Barcelona Lionel Messi ambapo ushindi huo wa mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia unaifanya Brazil kukaa kileleni mwa Bara la America Kusini kwa kufikisha alama 24 mbele ya Uruguay yenye alama 23 huku Argentina ikiwa katika nafasi ya 6 na alama 16.
halotel-1